Translate
Sunday, June 30, 2013
SEMINA:MAMBO YA KUTAFAKARI KABLA YA KUFANYA UAMUZI WA KUOA AU KUOLEWA
somo letu liko katika sehemu kumi na moja, Karibu tujifunze pamoja na Mungu akubariki.
Utangulizi
Ukifungua kitabu cha Yoeli.3:14 kinasema, “Makutano makubwa, makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku ya Bwana i karibu”. Huyu ndugu, mtumishi wa Mungu, aliyekuwa anaitwa Yoeli, Mungu alimpa nafasi ya kuona mambo ambayo yamekuwa yanafanyika tangu kuumbwa kwa ulimwengu, mpaka hapo Yesu atakaporudi tena. Anasema, ameona makutano makubwa, makutano makubwa, katika bonde la kukata maneno.
Tafsiri nyingine ya bonde la kukata maneno maana yake ni bonde la kufanyia maamuzi. Kukata maneno ni kufanya maamuzi. Sasa, bonde la kukata maneno, kwa tafsiri ya haraka ni dunia hii, wakati huu, mwanadamu anapoishi duniani.
Kwa sababu kabla hujazaliwa huna uwezo wa kuamua. Biblia inasema Mungu alimwambia Yeremia, “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, kabla hujatoka tumboni nalikutakasa” (Yeremia 1:5). Kabla hajawekwa tumboni mwa mama yake, Mungu alimjua Yeremia, ambayo inamaanisha Yeremia alikuweko, lakini alifananaje sijui! Lakini maandiko yananiambia ya kwamba alikuwepo na Mungu alimjua. Alipokuwa tumboni Mungu alimtakasa, maana yake alimtenga kwa ajili ya utumishi na wito wake.
Lakini Yeremia hakuwa na uwezo wa kuamua. Kabla ya kuzaliwa huwezi kuamua, baada ya kufa huwezi kuamua kitu chochote. Ndio maana tunatamani kila mtu lazima aokoke, aamue anataka kuishi maisha ya namna gani baada ya kufa, maamuzi hayo unayafanya kabla hujafa. Baada ya kufa hakuna mahali pa kufanyia maamuzi hayo tena!
Kwa hiyo kipindi hiki, ambacho mwanadamu anaishi ndicho kipindi cha kukata maneno. Bonde la kukata maneno ni dunia hii. Makutano makubwa; maana yake aliona watu wengi sana wamekaa katika bonde ambalo wanatakiwa kufanya maamuzi.
Katika dunia hii, (Kama ulikuwa hujafahamu afadhali ufahamu), ya kwamba kati ya jambo muhimu sana ambalo utawajibika nalo mwenyewe ni kufanya maamuzi. Na yako maamuzi ambayo unahitaji kuwa mwangalifu sana unapotaka kuyachukua, kwa sababu yatasababisha mabadiliko ya maisha yako kabisa.
Kwa mfano maamuzi ya kuokoka, kwa mfano maamuzi ya kumtumikia Mungu, yanabadilisha kabisa maisha yako, ndio maana Yesu anasema, mtu kabla hajamfuata, akae chini, ahesabu gharama; kuna gharama katika kumfuata Yesu, na kuna gharama katika kumtumikia Yesu. Maisha yako yanabadilika kabisa! Huwa saa nyingine mimi na mke wangu tunatamani kuishi maisha ya kawaida kama watu wengine, lakini haiwezekani, (watumishi wa Mungu wataelewa kitu ninacho elezea hapa), ukiishafanya maamuzi ya kusema unataka kumtumikia Mungu, maisha yako hayawezi kuwa ya kawaida tena, sio maamuzi madogo hayo.
Kuna maamuzi ya masomo, watu wanafanya mchezo wanapotaka kufanya maamuzi ya masomo, usifanye mchezo, ni maamuzi muhimu. Kuna maamuzi ya marafiki, unataka kuwa na marafiki wakina nani. Maamuzi haya yanaweza yakakubadilishia kabisa maisha yako. Lakini pia kuna maamuzi ya unachotaka kufanya maishani mwako ni nini. Mwingine atajitetea na atasema, Mungu anajua, - sawa Mungu anajua, lakini anahitaji maamuzi yako!
Wengine wanasubiri wakiishamaliza sekondari, au wakiishamaliza chuo kikuu, ndipo waamue wanataka kufanya nini. Ukiishafika chuo kikuu ndipo unataka kuamua cha kufanya maishani, utakuwa umechelewa. Kwa sababu, kama unataka kuamua kufanya kitu ambacho hukusomea, mambo yanawezayakawa magumu kwako, labda iwe ni Mungu anakupitisha hapo kwenye eneo hilo jipya.
Lakini pia kuna masuala ya kuamua kuoa au kuolewa, katika somo hili tutaangalia somo linalosema, “Mambo ya kutafakari kabla ya kufanya uamuzi ya kuoa au kuolewa”. Wengine mnaosoma somo hili ni vijana ambao umri wa kufikia kuolewa bado, lakini huu ni muda muafaka wa kukufikirisha jambo hili. Wengine wanaosoma somo hili wana karibia - karibia kuoa au kuolewa; au wameshaingia kwenye ndoa tayari. Halafu wanajikuta ya kwamba, afadhali wangekuwa wamejiuliza na kutafakari yaliyomo humu mapema zaidi.
Kwa muda ambao Mungu ametupa wa kuwahudumia watu mbalimbali katika miaka ya utumishi ambayo Mungu ametupa, kati ya jambo ambalo limesababisha maisha ya watu wengi yakawa mabaya au yakawa mazuri, yakawa magumu au yakawa marahisi, ni suala la kuoa au kuolewa.
Saa nyingine huwa ninawaambia vijana, Kama kijana anataka kuoa au kuolewa na ana haraka sana ya kutaka kuoa au kuolewa, basi asije kwangu kwa ushauri! Kama unataka kuoa au kuolewa, na una haraka sana ya kufanya hivyo tafadhali usije. Kwa sababu mambo niliyoyaona kwenye ndoa mbalimbali yananifanya hata mtu akija kwa ushauri wa kutaka kuoa au kuolewa, nimpitishe kwenye maswali magumu sana yatakayomfanya atafakari sana na kuomba kabla ya kuamua kuoa au kuolewa.
Nia niliyonayo ni ili nijue kama kweli amefikia mahali ambapo anajua kitu anachotaka kufanya. Maana wengi wanafikiri ni jambo rahisi. Mungu wangu aweze kukusaidia kuona ili usilichukuie jambo hili kwamba ni jambo jepesi, maana linabadilisha kabisa maisha yako
Mungu akuongoze, katika kuiendea ndoa
Mwl Sospseter Simon S. Ndabagoye
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.
Friday, June 28, 2013
BWANA ASEMA,YATOSHA, SASA NI WAKATI WAKE KUONEKANA.
Mlivyozunguka mlima huu,"Vyatosha"; geukeni upande wa kaskazini.Nawe, waagize watu,uwaambie,Mtapita kati ya mpaka wa ndugu zenu...nao watawaogopa....sitete nao,kwa maana sitawapa katika nchi yao kamwe...(Kumbukumbu la Torati 2:3-5)
Sijui, umekua katika hali hiyo uliyonayo kwa muda gani, wala sijui umehangaishwa na hiyo hali kiasi gani,ila leo Mungu anasema YATOSHA.
Pengine umeonewa sana, Umedharauliwa sana, Umetukanwa, Umekatishwa tamaa, Umebezwa kwa kila jambo, Umetemewa mate, Umechukiwa na hata Kutengwa na jamaa,Umepuuzwa mno, ila leo Mungu anasema"YATOSHA"
Haijalishi umeugua kwa muda gani, Umetafuta kazi pasipo kupata kwa muda gani,Umevumilia ili upate mwenzako kwa Muda gani? ila leo Mungu anasema "YATOSHA" Wakati wako wa kukumbukwa ni sasa, hata kama umeteswa na ulevi, uchawi,uzinzi,masengenyo n.k., Wee geuka upande wa pili, Mgeukie Yesu sasa, na hao adui zako watakuogopa, wala hawatakuwa na nafasi ya kuendelea kukutesa.
Hayo Magonjwa yatakuogopa, huo umalaya utakuogopa, adui sigara, pombe na wizi, vitakuogopa, wee geuka upande wa pili, mwangalie aliyekufa msalabani kwaajili yako, na hilo unaloliona tatizo kwako,litakuogopa hata litakukimbia.
Kama vile Mungu alivyowakumbuka Wanawaisraeli, walipokuwa wakiizunguka nchi ya Edomu,walipokuwa wamekufa moyo,wamekata tamaa,hata wakafikiria Mungu amewaacha, wengien wakadhani wamemtenda dhambi, hata wakaanza kukufuru na kulalamika (Hesabu 21:4-9). Hata wewe Mungu leo anaona maisha unayoishi, anaona changamoto unazokumbana nazo. Haijalishi ni kwa muda gani umekaa katika hali hiyo, ila Mungu anasema Yatosha, umefika wakati wake kuonekana katika maisha yako ikiwa utakubari kumgeukia na kufuata njia zake.
Hakika na kwambia,hutajuta kumgeukia,wala hutakuja kunyanyaswa ukimwamini.
NAKUTAKIA BARAKA ZA BWANA MAISHANI MWAKO, AKOMESHE MATESO YOTE,AONDOE ADHA ZA KILA NAMNA,ASIYE NA MTOTO APATE MTOTO,ASIYE NA KAZI APATE, AWAINUE KATIKA KAZI ZENU,BIASHARA ZENU, NA ZAIDI AWAJARIE AFYA NJEMA NA MAFANIKIO DAIMA.
KUOKOLEWA KWA NEEMA
Somo: Kuokolewa Kwa Neema
Watu wanaosema kwamba haiwezekani kuokoka duniani, wanasema hivyo, kwa sababu hawajui kwamba tunaokolewa kwa neema tu! Biblia inasema katika WAEFESO 2:8-9, “kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu (yaani zawadi kutoka kwa Mungu); wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu”. Tunasoma pia katika YOHANA 1:16, “Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema”. Iko siri kubwa iliyofichika katika maana ya neno, “Neema”.Kama sisi sote tungefahamu jinsi tunavyookolewa kwa neema, na jinsi tunavyopokea neema juu ya neema; kwa hakika, hakuna mtu hata mmoja ambaye angekwenda kwenye mateso ya moto wa milele. Wote tungekwenda mbinguni kirahisi sana, kwa kuwa tunaingia mbinguni, kwa neema tu; na Shetani asingepata mtu wa kukaa naye motoni, ila malaika zake tu, maana moto wa milele haukutengenezwa kwa ajili ya wanadamu, bali ulitengenezwa kwa ajili ya Shetani na malaika zake tu (MATHAYO 25:41).
Kwa bahati mbaya, nyakati hizi tunazoishi duniani mafundisho juu ya neema, yamekuwa nadra sana kupatikana katika majengo ya ibada. Watu wanaingia katika majengo ya ibada, miaka nenda, miaka rudi, bila kufahamu maana ya neema. Haikuwa hivi wakati Mtume Paulo alipokuwa akitenda kazi duniani. Nyakati za Mtume Paulo, karibu kila mtu alifahamu maana ya Neema. Ndiyo maana ulimwengu wote ulipinduliwa juu chini (MATENDO 17:6), na Shetani akawa katika hatihati ya kukosa wafuasi.
Iko siri kubwa iliyofichika katika maana ya neno, “Neema”
Wako watu wengi leo ambao wanaimba wimbo maarufu, “Neema, Neema, Neema, imefunuliwa”, lakina ukiwauliza ni nini maana ya neema, hawawezi kukujibu. Wako watu wengine ambano hukariri, na kusema kwa ufundi mkubwa sala ya Neema, “Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, na upendo wa Mungu Baba, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nasi sote, sasa na hata milele. Amen” (2 WAKORINTHO 13:14). Hawa nao ukiwauliza ni nini maana ya “Neema”, utashangaa kuona kwamba wengi kati yao, hawafahamu maana ya neema. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo. Ndiyo maana, mpendwa msomaji, Mungu, kwa makusudi kabisa, amekuletea “note” hii, ili tupate kujifunza kwa pamoja, maana ya neema, kwa jinsi ileile watu walivyojifunza, wakati wa Mtume Paulo. Ukisoma “note” hii hadi mwisho, hutakuwa jinsi ulivyo katika Jina la Yesu!
Nini basi, maana ya Neema? Ziko aina mbili za neema tunazozipokea kutoka kwa Mungu. Ndiyo maana tunasoma katika YOHANA 1:16, kwamba tunapokea “Neema juu ya Neema”. Aina ya kwanza ya Neema, ni upendeleo wa kuchaguliwa bila kuwa na sifa zinazostahili. Kwa kawaida, nafasi ya kazi nzuri, yenye mshahara mzuri inapotokea, mwajiri hutangaza nafasi ya kazi hiyo, na kuelezea sifa za mtu anayetakiwa kuajiriwa. Kwa mfano, mwajiri anaweza kusema, “Anatakiwa mtu aliye na digrii ya uchumi, na mwenye uzoefu wa kazi hii kwa muda usiopungua miaka mitano. Awe na umri wa miaka 40 au zaidi, na mwenye haiba nzuri. Mtu mwenye uwezo wa kutumia kompyuta, atafikiriwa zaidi”. Baada ya watu kusoma au kusikia tangazo hili la kazi, wengi hutuma maombi ya kazi. Hatimaye watu mia mbili au zaidi wanaweza kuchaguliwa kwenda kwenye mahojiano au “interview”, na kati yao mtu mmoja tu mwenye sifa za hali ya juu kuliko wengine wote, ndiye atakayechaguliwa.
Sasa basi, kuokolewa na kuhesabiwa haki ya kuingia mbinguni, ni kitu cha thamani kuliko kazi yoyote ile, hata ingekuwa na mshahara mkubwa kiasi gani. Hata tukiwa na kazi nzuri yenye mshahara mkubwa, siku moja tutaiaga dunia hii, na kuiacha; na tukiwa tumeishi dhambini, mshahara, wetu utakuwa mauti ya milele, yaani kutupwa katika mateso ya moto wa milele (WARUMI 6:23). Lakini ikiwa tumeishi maisha yanayompendeza Mungu, tutaokolewa kutoka katika mateso hayo, na kuishi na Mungu mbinguni, kwenye raha isiyo kifani; milele na milele. Sasa basi, Mungu anachaguaje watu wa kuingia mbinguni? Je, anaangalia sifa au matendo yao? Jibu ni la. Tulisoma, na tunasoma tena katika WAEFESO 2:8-9, “Kwa maana mmeokolewa kwa neema,…….. wala si kwa matendo”. Hatuokolewi kutokana na matendo yetu tuliyoyafanya kamwe.
Kutokana na matendo yake, hakuna mwanadamu yeyote mwenye haki, mbele za Mungu (WARUMI 3:20). Tangu mwanzo kabisa mwanadamu amekuwa akimhuzunisha Mungu kwa maovu yake kiasi ya kumfanya Mungu kughairi kwa nini amewaumba wanadamu. Katika MWANZO 6:5-7, “BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani, kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya”. Baada ya maneno haya, Mungu aliwaangamiza wanadamu wote kwa Gharika, kasoro watu wanane tu, Nuhu na jamaa yake. Wakati wa Musa, vivyohivyo, Mungu alitaka pia kufuta kabisa kizazi cha Waisraeli, na kubaki na Musa peke yake; kama siyo maombi ya Musa (HESABU 14:11-20). Katika vizazi vyote, Mungu anatoa ripoti ifuatayo juu ya maisha ya wanadamu, “Wote wamepotea, wameoza wote pia; hakuna mtenda mema la! hata mmoja” (WARUMI 3:12). Katika wanadamu wote, waliowahi kuishi duniani, ni Yesu Kristo tu aliyeishi duniani bila kufanya dhambi.
Ni Yesu Kristo tu aliyeishi duniani, bila kufanya dhambi. Siku zote, Yesu Kristo alifanya yale yanayompendeza Mungu (YOHANA 8:29). Alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote bila kutenda dhambi hata moja (WAEBRANIA 5:14-15). Huyu pekee ndiye Mungu anayemtaja akisema, “Huyu, ni Mwanangu mpendwa wangu, ninayependezwa naye” (MATHAYO 3:17). Sasa basi, sisi wanadamu tunaokolewa siyo kutokana na matendo yetu bali kutokana na matendo ya Yesu Kristo. Tunachotakiwa kukifanya ni kumwamini Yesu tu na kuifurahia kazi ile aliyoifanya msalabani, pale alipochukua adhabu iliyomstahili Baraba, mfungwa mashuhuri. Baraba akafunguliwa na Yesu akachukua adhabu yake ya kifo (MATHAYO 27:16-17, 20-26). Sisi nasi ni wahalifu, wenye dhambi kama Baraba, na tunaokolewa kutoka katika adhabu ya mauti ya milele, yaani mateso ya moto wa milele, kwa imani tu, katika adhabu aliyoichukua Yesu kwa niaba yetu.
Tungeweza kusema kwamba Baraba, mtu mhalifu, aliwekwa huru au aliokolewa katika adhabu ya kifo kwa neema tu! Hakustahili! Kutokana na Yesu kuchukua adhabu hiyo, Baraba akawa huru. Vivyo hivyo, kutokana na Yesu kumpendeza Mungu sikuzote, sisi nasi tunahesabiwa haki ya kuingia mbinguni alikokwenda, kwa imani tu katika Yeye! Kazi njema aliyoifanya Yesu, imetupa kuirithi mbingu aliyokwenda bila sisi kuifanya. Ni kama jinsi ambavyo katika mambo ya dunia, bondia anavyopigana ulingoni kwa shida kubwa, na kisha akishinda na kupewa mamilioni ya fedha; mke wake aliyebaki nyumbani bila kupigana, naye anakuwa milionea! Hii ndiyo Neema! Yesu Kristo, ndiye aliyepigana na Shetani na kumshinda pale alipomjaribu kufanya dhambi, na sisi tunahesabiwa kushinda katika Yeye Yesu, kwa imani tu! Ndiyo maana Biblia inasema katika WAEFESO 2:8-9, “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu (Zawadi ya Mungu), wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu”.
Kwa hiyo tunachotakiwa kukifanya, ili tuokolewe, ni rahisi sana. Tunatakiwa kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha, na kwa imani tu, katika Yesu Kristo, tunahesabiwa mara moja haki ya kuingia mbinguni. Hiyo ndiyo neema ya Kwanza. Aina ya pili ya Neema, ni msaada utokao mbinguni, wa kutuwezesha kufanya mapenzi ya Mungu. Kama tulivyoona, hatuokolewi kutokana na kujitahidi kufanya hili au lile, bali ni kutokana na kazi aliyoifanya Yesu, siyo sisi. Vivyo hivyo, kutokana na upendo wa Mungu, Mungu anajua pia kwamba hatuwezi kufanya mapenzi yake mpaka atupe msaada wa kutuwezesha kufanya hivyo. Biblia inasema katika TITO 2:11-12, “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi na haki, na utauwa (utakatifu), katika ulimwengu huu wa sasa”. Bondia akishinda na kuwa tajiri, mkewe naye hutajirika bila kupigana
Mtu anapofundishwa kuendesha gari, kwa lugha nyingine, huwa amewezeshwa kuendesha gari. Vivyo hivyo, Neno la Mungu linaposema kwamba neema iliyofunuliwa ndiyo inayotufundisha kuishi maisha ya utakatifu katika ulimwengu huu wa sasa, maana yake neema ya Mungu, ndiyo inayotuwezesha kuishi maisha ya utakatifu. Maisha ya wokovu ni ya kuwezeshwa kufanya mapenzi ya Mungu, siyo kufanya mapenzi ya Mungu kwa kujitahidi kwa nguvu zetu. Biblia inasema katika WAKOLOSAI 1:10-11, “Mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake…..” Tunayaweza yote katika Yeye Yesu atutiaye nguvu (WAFILIPI 4:13). Nguvu hii ndiyo Neema ya pili. Baada ya kuokolewa, tunawezeshwa kufanya mapenzi ya Mungu. Tunachotakiwa kufanya, kwa kila mapenzi ya Mungu tunayoelekezwa kuyafanya katika Neno lake, tunakikaribia kiti cha neema cha Mungu na kuomba neema au msaada wa kutusaidia kufanya mapenzi yake (WAEBRANIA 4:16).
Mpendwa msomaji, unaona sasa! Hakuna haja ya kusema, “Hivi kweli nitaweza kushinda dhambi duniani? Hivi kweli maisha ya wokovu nitayaweza?” Ni Neema juu ya Neema. Unalotakiwa kufanya ni kutubu dhambi zako tu kwa kumaanisha kuziacha; kwa imani tu, na mengine yanayofuata mwachie Yesu; na leo hii utashangaa kuona maisha yako yamebadilika ghafla na kwa urahisi utaona unaweza kufanya mapenzi ya Mungu, bila jitihada za kibinadamu. Je, uko tayari kutubu dhambi zako? Najua uko tayari. Basi sema hivi, “Mungu wangu, natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha kuanzia leo. Asante kwa neema yako ambayo kwa hiyo tunaokolewa kutokana na kazi aliyoifanya Yesu. Niokoe sasa na kunipa neema ya kufanya mapenzi yako kuanzia sasa na wakati wote ujao. Asante kwa kuniokoa katika Jina la Yesu. Amen”. Ili uzidi kuukulia wokovu ulioupokea leo, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!
Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook, Twitter, n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe. UBARIKIWE NA BWANA YESU!!

Somo: Kumtafuta Bwana Mungu.
Lengo Kuu la Somo: Kutambua umuhimu wa neno la Mungu kwetu, umuhimu wa maombi na kujifunza kumtumikia Bwana.
Lengo Mahususi: Kutambua umuhimu wa kumtafuta Mungu, njia ya mwanadamu kumtafuta Mungu yaani Dini na namna Mungu anavyomtafuta Mwanadamu kupitia Wokovu.
Matarajio: Msomaji, kupata uelewa wa kutosha juu ya kumtafuta Mungu na kuwa mwanafunzi Bora wa Yesu Kristo. Namwomba Roho Mtakatifu, asikuache bila kukuhudumia wewe,unayesoma ujumbe huu, Bwana asikupungukie katika shughuli zako,muda huu aulipe kwa wingi wa hekima zake. Usipotee bure Muda huu; kwa jina la Yesu.
Utangulizi.
Neno la Mungun ni Muhimu sana katika maisha yetu, sisi kama viumbe wa Mungu, aliowaumba kwa mpango maalumu wa kiutawala pamoja na yeye. Ifahamike kuwa, “mtu” ni mwili, roho na nafsi. Mtu kama yu hai, maana yake anayo roho, na kama mtu ana roho, ni dhahiri kuwa anamwili, kwa maana, maandiko yanasema wazi kuwa, “Roho, huupa mwili uha”i, na “mwili ndilo hekalu la Roho”.
Kwa kuwa mwili, umejengwa kuwa dhabahu la Roho, kumbe mtu anenapo, basi huyo ni Roho ananeye, awe roho wa Mungu, au wa shetani! Kikubwa hapa, ni kujua kuwa, mwanadamu, huongozwa na uwezo mkubwa wa kiroho, ambao matunda yake, hutuonesha kuwa, roho huyo ni wa MUNGU au la. Ndiyo maana maandiko yanaeleza wazi kuwa, “ulimi hunenana yaujazayo moyo”. Ina maana kuwa, kuongea,huanzia ndani kabla ya kutokeza nje, hushuhudiwa na nafsi.
(1) Roho na Mwili, kipi bora zaidi?
Kwa mtazamo huo tulipata kwatika utangulizi, yatupasa kujua kuwa, kama vile mwili unavyohitaji kula vizuri, kuvaa vizuri, kulala na kupumzika, kuburudika kwa nyimbo na hata sherehe mbalimbali; Roho yako,ni zaidi. Ndiyo maana, maandiko yanasema, “Linda moyo wako,kuliko yote uyalindayo “. Hapa tunapata kujua kuwa, “roho ni bora kuliko mwili”. Kwamaana, mwili, hutoa matokeo ya kilichofanywa na roho. Kwa maneno mengine, ukiona mtu anatukana, jua kuwa, yale ndiyo matokeo ya Roho aliye ndani yake. Kadharika, kama mtu ni mgomvi daima, huyo ndiye roho aliye ndani yake! Je, hujawahi kuona hata watumishi wa Mungu wanasemana na kutupiana vijembe? Basi ndizo roho zinenazo ndani yao.
Zingatia: “Ninachotaka ujifunze hapa ni kuwa, yale ufanyayo, ni uthihirisho wa roho aliyeko ndani yako” hivyo, kama watoto wa Mungu, tunapaswa kuuthilishia umma, kuwa, tunaye roho wa Mungu kwa matendo yetu, wala si kwa kusema tu. Kumbuka neno linasema” imani pasipo matendo imekufa” je, yafaa nini tukiwa na imani pasipo matendo? Daima, tunapaswa kuwa na matendo mema,yatakayothirisha uwepo wa roho wa Mungu ndani yetu.
(2) Roho anapaswa kulelewaje?
(a) Kulishwa neno.
Ndugu yangu, roho aliyeko ndani yako, anapaswa kulishwa vyakutosha. Biblia inasema, “Neno la Mungu ni chakula cha roho” tena “neno la Mungu ndiyo uzima” kumbe, ili tupate uzima, ni lazima huyu Roho ashibishwe vya kutosha kupitia maandiko matakatifu ya Mungu yaitwayo Biblia( Rejea, karatasi ya kwanza na ya pili kwenye Biblia yako inaeleza maana ya Biblia).
Kwa kigezo hicho, yafaa sana, mtu apate mafundisho kwa wingi sana ili aupe mwili uhai. “Roho ndiye autiaye mwili uhai” Hii inamaana kuwa, Roho ikifa, na mwili hupoteza uhai wake. Kumbe yatupasa kuijali sana Roho kuliko mwili.
Kwa jinsi ya mwili, mtu hupenda kuulisha mwili zaidi kuliko Roho, na mwili unapotaka kulishwa hudai hata kwa nguvu. Hata kama uko safarini, mwili hupata chai, hupata maji,hupata chakula na wakati mwingine huzidisha unapokuwa nyumbani, mara mishikaki, mara uji, mara juice. n.k. mwili unapopata hitirafu kidogo, hututibiwa haraka haraka, tena wengine hushituka sana, juhudi juu ya kuukokoa mwili huwekwa pamoja, majirani hushiriki, ndugu, marafiki na hata wapiti njia tuu, hushiriki katika kuhakikisha mwili unakuwa salama. Je, roho tunaijali kweli? Ebu fikiria kwa leo tu, umafanya mangapi kwaajili ya mwili? Umepiga mswaki, umeupaka mafuta,umeuvika, umeupa chai na hata milo yote, umeupumzisha; lakini swali ni je, umeridhika, kesho hautadai? Roho je, umeilisha, umesoma neno la Mungu mara ngapi? Ni mara ngapi umesali licha ya kuombea chakula na kujihami kwa kusema “Mungu wangu!” kwa kushituliwa na gari lililotaka kuugonga mwili huo?
Ndugu yangu, neno la “Mungu ni tamu kuliko asali”(Zaburi 19:11,Mithali 24:13), au pengine niseme, ni tamu kuliko kile chakula ukipendachom zaidi. Tamani sana kuwa na neno la Mungu la kutosha moyoni mwako, Yesu alimshinda shetani kwa neno, na lazima ujue kuwa asili / chanzo cha kila kitu ni neno (Yohana 1:1&3) na pasipo huyo neno,hakuna kilichofanyika. Kumbe, afya inatoka kwa neno, mke/mme mzuri anapatikana humo kwenye neno, utajiri unapatikana humo humo, mali na fedha unavyotamani,watoto wazuri vimeumbwa katika neno! Kwa maana hiyo, ni neno tu, linaweza kukupa haja ya moyo wako.
(b) Kulishwa maombi.
(Mithali 8:17&18),”Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidiiwataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu; naam, utajiri udumuo, na haki pia” pia (Luka 18:1-6) utabaini kuwa, tunapaswa kudumu katika maombi, na kupitia maombi ya kila mara,basi utaona Mungu akikujibu kwa kadri unavyoonesha kuomba kwa bidii. (Yakobo 5:16b) “kuomba kwa mwenye haki,kwafaa sana,akiomba kwa bidii”. Hii inamaana kuwa, unapaswa,kuijaza roho maombi kwa wingi mno. Kupitia maombi haya, basi yatamgusa Mungu kama tulivyoona katika (Luka18:6), naye atakujibu kwa kadri ya maombi yako.
(3) Je, dini inaweza kumfurahisha roho?
Ndugu yangu, napenda kukujuza siri hii, itakusaidia, “Dini” kamwe haitampeleka mtu mbinguni, wala hakuna mbingu ya Dini. Kwa kuwa, mtu wa Dini ni mtu wa sheria tu, je sheria zitatupatia mbingu? Ikumbukwe kuwa, Dini ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu. Katika kumtafuta huko, mwanadamu hujiwekea utaratibu anaouona utamsaidia kuyaendea makusudi yake ya kumtafuta Mungu wake. Hata hivyo, huweka kitu anachokijengea imani kuwa ndicho sahihi, na kukifuata,na kwa hali hii, hupinga uongozi wa roho na kufuata maongozi ya mwili. Je, mwili unaweza kukufikisha mbinguni, je mwili huu utaiona mbingu, au tutavikwa miili mipya? Je si maandiko yamesema juu ya kuilinda roho kuliko yote tuyalindayo, kwa kuwa hapo ndipo urithio wetu ulipo?
(4) Wokovu ni nini kwani?
Hata hivyo, inakupasa kujua kuwa, Wokovu ni mpango wa Mungu katika kumtafuta mwanadamu. mpango huu ulianzia kwenye kuzaliwa kwa Yesu na kuutimiza katika kifo chake msalabani. Na hapo ndipo, tunapopata uzima wa milele ambao ni uzima wa roho, yaani uzima ulio nje ya mwili. Uzima usiochujuka, uzima udumuo,uzima imara, uzima unaodumu milele yote.
(5) Yatupasa kufanya nini?
(a) Mungu anakutaka umrudie.
Ndugu yangu, uzima huu, unapatikana, kikubwa, ni kukubali kuwa chini ya uongozi wa Roho mtakatifu, ukubali ukombolewe,utoke chini ya sheria kwa kuwa sheria haitakufikisha popote, sheria ni ya mwili tu, sheria inaisha mwili uishapo,lakini neema inadumu milele na milele. Mtafute leo Mungu kwa bidii, nawe utampata,atakuwa Bwana na mwongozi wako (Mithali 1:4&5). Ukisoma (Isaya 55:6-8), “Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana. Mwiteni, maadamu yu karibu. Mtu mbaya na aiache njia yake mbaya, na asiye haki,aache mawazo yake. Na amrudie Bwana naye atamrehemu; na arejee kwa Mungu wetu. Maana mawazo tangu si mawazo yenu, na wala njia zenu si njia zangu, asema Bwana”. Maneno hayo, yanatudhihirishia kuwa, kwa njia zetu kama wanadamu, kwa taratibu zetu na miongozo yetu,hatuwezi kumpata Mungu, bali tuziache njia zetu, tumtafute yeye, naye ataturehemu na kutuokoa.
(b) Mungu hupatikana katika roho.
Tunaweza kumpata Mungu katika maombi tu. (Yeremia 29:12-14) nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. Nanyi mtanitafuta na kuniona mtakapo nitafuta kwa moyo wenu wote; nami nitaonekana kwenu, asema Bwana. Mungu hawezi kuonekana kwa njia za kibinadamu, kwa sheria za mwili, bali kwa kudumu katika maombi na kuutafuta uso wake, kupitia uongozi wa Roho.
(c ) Kubabudu katika roho ni ishara ya kuwa na Mungu.
(Yohana 4:23&24) Lakini saa inakuja, nayo saa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni roho, nao wamwabuduo, inawapasa kumwabudu katika roho na kweli.
(c) Ukimwacha Mungu, naye anakuacha.
Nawe Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, umkaribie, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa Bwana hutafuta-tafuta mioyo yote , na kuyatambua mawazo yote ya fikira, ukimtafuita, ataonekana nawe; ukimwacha atakutupa milele. (1Nyakati 28:9). Pia ukisoma (2Nyakati 20:1-21) utaona Yehoshafati alivyomtafuta Bwana, alipokabiliwa na vita dhidi ya mahasimu wake, lakini alipoamua kumtafuta (mstari wa 3) alimwona na alimtetea.
Ndugu yangu, nakusihi umpende Mungu, na uwe tayari kumrudia naye atakuwa tayari kukupokea, ataibadirisha historia ya Maisha yako, tunavyoongea, atayabadiri na kuwa mapya. Haijalishi umetumia akili yako kiasi gani,katika kuhakikisha ndoa yako inasitawi, haijalishi umehangaika kiasi gani ili kuhakikisha, unafanikiwa kimaisha na hata katika masomo yako! Pengine, biashara yako, imekuhangaisha sana, ebu leo sema yatosha, sasa Mungu nakutaka wewe uwe kiongozi wangu.
Mwl. Sospeter Simon S. Ndabagoye.
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.
Box 1275,
Tabora.
E-mail: sos.sesi@ yahoo.com
SOMO: JIFUNZE KUFUMBA MACHO.
Lengo kuu: Kuacha Dhambi.
Lengo Mahususi: Kila mtu,kuacha Dhambi na kuwa mwanafunzi wa Yesu, kumpenda Mungu peke yake, na kuziacha njia nyingine.
Utangulizi.
Ndugu zangu, napenda niwakaribishe katika somo letu fupi sana, ambalo kwa hakika, nina imani Mungu hatakuacha umalize kusoma ujumbe huu, bila kukuhudumia. Na wala, hata acha kukulipa muda huu, unaoutumia kujifunza maneno haya, hata ukaacha kufanya kazi nyingine, na kuuachilia mwili,fikra na mawazo hata pesa yako, ili uweze kusoma ujumbe huu; Mungu akubariki sana.
Napenda kukushirikisha juu ya haya hili neno “Kufumba Macho”
Ni wazi kuwa, kila mara, katika maeneo mbali mbali, huwa tunafumba macho mara tunapotaka kuomba”haleluya”. Utaratibu huu, ambao umefanywa kuwa kanuni, mara zote hufanywa kwa lengo la kuvuta umakini na hisia kwa Mungu. Njia hii, humfanya mtu, atulie kimawazo na hata kiakili. Kwa kujitenga na ulimwengu na mambo yanayopita katika upeo wa macho yake.
Aidha, kufunga macho humfanya mtu, asibugudhiwe na vitu vinavyopita mbele yake, ambavyo vinaweza kumhamisha kimawazo, na kumfanya ashindwe kuomba vizuri. Wakati mwingine, inapotokea kitu cha kutisha, mtu hufumba macho, ili asiendelee kuona kicho kitu kinachokuja mbele yake, ambacho pengine kitamtoa katika msimamo wake.
A. JE, KUFUMBA MACHO MAANA YAKE NI NINI HASA?
****Kiimani, kufumba macho, ni zaidi ya kuacha kuona, kwa maana hata kipofu, haoni ila anaweza akawa hajafumba macho. Kufumba macho, ni hali ya “kuacha dhambi” na kuamua kuiacha kabisa, na kumtafuta Mungu. Kumwangalia Mungu tu.
****Kuokoka, ni kufumba macho; kuamua kujikabidhi kwa Mungu, siyo suala la mchezo, kwani mwanadamu anapookoka, wakati jina lake linaandikwa katika kitabu cha uzima, hata kuzimu huandikwa kwa kuwa ametangaza vita na shetani. Si maanishi kuwa mtu asiokoke, eti kwa kuogopa kuwa katika vita na shetani, la hasha! Ndiyo maana biblia inasema, “je, twendelee kutenda dhambi kwa kuwa neema ipo, hasha” lakini pia, kumbuka pia, ahadi za Mungu kwetu kuwa, “hii vita tunayopigana si ya kwetu, bali ni yake yeye mwenyewe”(2Nyakati 20:15), tena, imetupasa, kumwamini yeye kwakuwa, yu na nguvu zaidi ya huyo adui yetu (Kutoka 14:13, Kumb1:29&30, 2Nyakati 32:7).
****Kuacha dhambi, ni kufumba macho” ebu fikria, mwanadamu ambaye kiasili, anaishi kwa kuiba, kutapeli, kufanya ukahaba, kunyang’anaya n.k. mtu huyu, ameifanya dhambi kuwa sehemu yake ya kutafutia maisha, kuacha kazi hiyo si jambo la masihala, ni jambo linalihitaji ujasiri. Inahitaji nguvu ya Mungu, na hapo ndipo tunapoomba Mungu sana atusaidie.
****Kuacha ulevi, ni kufumba macho, mtu aliyezowea kunywa pombe, kuvuta sigara, bangi na vileo vinginevyo, kuviacha si mchezo. Mtu aliye athiriwa na madawa ya kulevya, kuyaancha mpaka nguvu ya Mungu imshukie.
****Kuacha uchawi, ni kufumba macho, kwa hali ya kawaida, mwanadamu aliyeweka tumaini juu ya nguvu za kipepo, kuziacha huwa ni vigumu sana, kwa kuwa, huyo ndiye mungu wake, anayemtumikia, hata hivyo kumchomoa katika imani hiyo, si jambo la lelemama, inahitaji uweza wa Mungu.
****kuacha umbeya, kuseng’enyana ni kufumba macho. Mtu aliyezowea kusemana wenzie, hata akilala, huota anasutana, huota anamsema mwenzake, hata akiwa anahubili, atatoa mifano inayowahusu wengine, si kwa lengo la kujenga, bali kubomoa, mwanadamu mwenye tabia hii, kuacha tabia hii, inahitaji nguvu ya Mungu.
***Kumpenda mke/mme wako kwa dhati ni kufumba macho, suala la kupenda, ni suala amabalo lipo kila siku na halijafungiwa kikomo, hivyo, mtu kumpenda mke/ mme wake kwa dhati, kama ilivyoamuliwa ni kufumba macho. Kutokuwaona hao ma”handsome” na ma“beautiful” wapya, kuwaacha madogodogo, maserengeti boys, ni kufumba macho.
B. KUMTUMIKIA MUNGU NI KUFUMBA MACHO?
****Lakini, ndugu msomaji, inabidi ujue kuwa, kumtumikia Mungu pia ni kufumba macho, kumtii na kuzishika amri zake, ni kufumba ,macho, wala siyo kwamba na kutisha, lazima ifike mahali ujuwe kuwa, unapoamua kumtumikia Mungu, si suala la kulala na kuamka, kama unavyoweza kuamua kujenga banda la kuku; Yesu mwenyewe alisema; “kama unataka kunifuata mimi, sharti, ujikane, ujitwike msalaba ndipo umfuate” tena akasema, unapaswa kuhesabu gharama halisi” na ukimfuata, sharti, usiwe wa kugeuka geuka nyuma. Tena anasema, hapendezwi nao wenye nia mbili. Kuna wakati, unapita katika majaribu,ndugu wanakutenga na pengine unabaki peke yako, hata mimi nimepita katika hali hizo, lakini inakupasa uwe na ujasiri, usimamie iliyo kweli daima, hata kama unauma. “Kuwa tayari, kuvumilia uchungu wa ukweli, kuliko kufurahia, utamu wa Uongo”. Na hapa ndipo Joshua aliposimama na kutangaza hadharani” ….lakini Mimi pamoja na nyumba yangu, tutamtumikia Bwana” (Yoshua 24:15)
****Kutii sauti ya Mungu, ni kufumba macho, Kumbuka kuwa, wakati Mungu anatoa maelekezo juu ya njia unayopaswa kuiendea, shetani pia, huingilia kati na kutoa maelekeza yake, mara zote, shetani hitoa maelekezo yanayofaa machoni pa mwanadam, hulaghai kwa sauti nyololo na kukuonesha mambo mazuri na matamu. Angalia nyoka alivyomdanga Hawa na kuyaacha maagizo ya Mungu, akayaangalia matunda yapendezayo mtini, na kuyala (Mwanzo 3:1-7). Lakini, hata Yesu mwenyewe alidanganywa na Ibilisi mara kibao, ashukuriwe aliyejuu, Yesu, hakuangalia mkate wala miliki za dunia, alifumba macho na kuiangalia mbingu mpaka mwisho.
****Kutoa sadaka nikufumba macho! Maandiko matakatifu, yanatueleza juu ya kumtolea Mungu sehemu zilizo nona, na kupitia matoleo yetu,ndipo Baraka hufunguliwa kwetu. Hata hivyo, imekuwa ngumu kulitii andiko hili, ndiyo maana, ni vigumu kwetu kumtolea Mungu matoleo mazuri, badala yake tunatoa masalia. Haikuwa lahisi kwa Ibrahim kumtoa Isaka, huku anajua ndiye mwanae wa pekee na mrithi wake. Isipokuwa, ilimpasa afumbe macho, na hapo ndipo alipobarikiwa (Mwanzo 22:1-15)
****Kuitii sauti ya Mungu mpaka mwisho, nikufumba macho, ndiyo maana mtu hupita katika majaribu makubwa na mazito, magumu na ya kutisha ila unapaswa kufumba macho, kumbuka neno la Mungu linasema “atakayevumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka” hata wewe unapaswa kuvumilia mpaka, mwisho,usione hatari hata kufa kwa kuisimamia kweli, kwanini udanganye, au umkane Yesu kwa kitu kidogo, leo mtu yuko tayari kubadiri dini kwasababu ya ndoa tu, kwanini unaufanya ukristo kuwa bei chee kiasi hiki. Akina Meshaki, Shadraki na Abednego, wako wapi leo, watu waliokubali kufa kwaajili ya Mungu. Watu wenye imani kama Elia, leo wako wapi?
Pengine Muda unaweza usitutoshe kumaliza somo letu, kama umebarikiwa, uweze kushare ujumbe huu, ili kuifanya kazi ya Mungu, usishangae ukiona watu hawacomment, pengine wameamua kuufanyia kazi ujumbe huu kimya kimya. Mungu akubariki sana.
Na.
Mwl. Sospeter Simon S. Ndabagoye
New Elshaddai Ministrie NEM-Tanzania.
USHUHUDA MZITO HUO.
JIANDAE KUKUTANA NA MUNGU WAKO! FALME ZA MBINGUNI
NA KUZIMU, NA KURUDI KWA KRISTO NA Angelica Zambrano Imefasiriwa na Alpha
Wilson Magubila kwa
Neema aliojaliwa na Mungu
NA Angelica Zambrano Imefasiriwa na Alpha Wilson
Magubila kwa Neema aliojaliwa na Mungu
Kwa kipindi cha masaa 23, binti mdogo wa ki-Ecuado
aitwaye Angelica alioneshwa falme za Mbinguni na Kuzimu, na kurudi kwa Kristo
mara ya pili. Alishuhudia Yesu akilia kwa huzuni aonapo umati wa roho
zilizopotea milele, ulimwengu uliomkataa yeye, kanisa lisilo tayari kabisa kwa
ujio wake, watu wameacha kushuhudia kwa walipotea mbali na kweli, na anasa za
dunia zimeteka hata watoto kwa shetani. Alishuhudia watu maarufu wakiteswa
katika moto, waimbaji, wanamuziki na hata Papa. Angelica alioneshwa jinsi
ufalme wa Mbinguni ulivyoandaliwa kwa uzuri na utayari, utukufu usioweza
kufikirika, ambapo hakuna uovu. Japokuwa Yesu anakuja kwa ajili ya watakatifu
tu; wengi wa wana wa Mungu hawatakuwa tayari kwa siku ile, na wataachwa nyuma
katika ulimwengu utakaogawanyika vipande vipande. www.DivineUfunuo.info/23 (Mahojiano kwa video, mwanzoni ni kwa lugha ya Kihispania,
huko El Empalme, Ecuador. Sept. 29, 2009).
Maxima (Mama yake Binti):
Jina langu ni Maxima Zambrano Mora, tunasali kanisa la
"Casa de Oracion" huku El Empalme. Tulikuwa katika kufunga kwa siku
15, na kulia kwa Mungu. Binti yangu Angelica aliungana nasi pia. Katika kipindi
hicho cha siku 15 cha kufunga, niliweza kupata maono zaidi ya asili, ambayo
sijawahi kuona kabla. Tulikuwa tunaomba na kufunga katika kipindi maalumu cha
kumtafuta Bwana, tuliendelea kuomba na kulia pale nyumbani, tukisubiri Mungu
aseme nasi. Bwana alitutia matumaini makubwa sana. Kwaajili ya majaribu yetu
tulikaribia kukata tamaa, lakini Bwana alikuwa pamoja nasi kutusaidia. Alitupa
neno la Yeremia 33:3 "Niite, nami nitakuitikia, ame nitakuonesha mambo
makubwa, magumu usiyoyajua.” Binti yangu alitia msisitizo sana katika neno hili
kwa Bwana, japokuwa sikujua kwa wakati huo.
2
Angelica (Binti Mhusika):
Jina langu ni Angelica Elizabeth Zambrano Mora. Nina
umri wa miaka 18, na ninasoma chuo cha "Colegio José MarÃa Velazco
Ibarra", hapa El Cantón, El Empalme, Ecuador. Kwanza nilimpokea Kristo
nilipokuwa na umri wa miaka 12, lakini nalijiambia mwenyewe, "Hakuna hata
mmoja wa rakifi zangu aliyeokoka na nikajisikia aibu miongoni mwao", kwa
hiyo nirudi nyuma mbali na Mungu na kuishi maisha mabaya. Lakini Mungu
alinivuta nitoke huko. Siku ya sherehe ya kutimiza miaka 15, nirejea tena
kupatana na Bwana, lakini nia haikutulia sawa sawa. Biblia inasema (Yakobo
1:8), "Mtu wa nia mbili husita-sita katika nia zake zote" na mimi
nilikuwa sawa na mtu huyu. Baba yangu aliwahi kusema "Hutakiwi kuwa hivyo,
siyo vizuri, ni vibaya mwanangu" lakini nalimjibu, "Hivi ndivyo nilivyo,
nataka kuwa hivyo, hakuna mtu wa kuniambia namna nitakiwavyo kuwa, wala
chakufanya, wala namna ya kuvaa, au mwenendo." Naye alijibu, "Mungu
atakushughulikia na atakubadilisha wewe."
Siku ya sherehe ya kutimiza miaka 17, nilimkaribia
Bwana. Tarehe 28 mwezi Aprili nilimwendea Bwana na kumwambia, "Bwana,
nijisikia vibaya sana, najua kuwa mimi ni mwenye dhambi” na nilimweleza jinsi
ninavyojisikia. "Bwana, nisamehe mimi. Natamani uandike jina langu katika
kitabu cha Uzima na unipokee niwe mwanao." Nilitubu na kutoa maisha yangu
kwa Bwana rasmi. Nikasema “Bwana, naomba unibadilishe, ufanye tofauti ndani
mwangu." Nililia kwa moyo wangu wote, huku nikimwomba Bwana anibadilishe
mimi. Lakini kwa kadri ya muda ulivyozidi kupita, sikuona madiliko yoyote.
Badiliko pekee nikuwa nilianza kuhudhuria kanisani, kusoma biblia na kuomba.
Hayo tu ndiyo mabadiliko katika maisha yangu.
Ilipofika mwezi Agosti, nilikaribishwa katika mfungo wa
siku 15. Niliamua kushiriki, lakini kabla ya kuanza nilisema: “Bwana, naomba
unishughulikie hapa." Katika kipindi chote cha mfungo, Bwana alikuwa
anasema na karibu kila mtu, kasoro mimi tu! Ilikuwa kama vile Bwana hajaniona,
na hilo liliniumiza sana. Nikaomba, "Bwana, hutanishughulikia mimi?"
Nikaomba na kulia peke yangu na kusema tena, "Bwana, je unanipenda? Je upo
hapa? Upo nami hapa? Kwanini husemi nami kama unavyosema na kila mmoja hapa?
Unasema mambo mengi kwa wenzangu, hata maneno ya unabii, lakini siyo
kwangu" Nilimwomba ishara ya kuwa yu nami, na Bwana akanipa neno la
Yeremia 33:3, "Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonesha mambo makubwa,
magumu usiyoyajua." Nikasema, “Bwana, je umesema nami?” Kwasababu
nilisikia sauti yake na kupata maono ya maneno yaliyoandikwa katika Yeremia
33:3.
Nikasema “Bwana, hiyo ni kwaajili yangu?” Nilitunza na
kukaa nalo kimya mwenyewe wakati kila mmoja akishuhudia waliyopewa na Bwana na
kuoneshwa. Lakini mimi nilitunza siri yangu na mara kwa mara nilijikumbusha na
kutafakari maneno: " Niite" maana yake nimwombe, lakini nini maana
ya: "mambo makubwa, magumu" niliwaza, “Huenda ikamaanisha Mbinguni na
Kuzimu." Kwa
3
hiyo nalimwambia “Bwana, naomba unioneshe Mbinguni tu,
lakini siyo kuzimu, kwasababu nimesikia kuzimu ni sehemu ya kutisha na mbaya
sana." Lakini baadaye nikaomba kwa moyo wangu wote, "Bwana kama ni
mapenzi yako kunionesha, na iwe hivyo, lakini nibadilishe kwanza. Naomba ufanye
tofauti ndani mwangu, nataka kuwa tofauti.”
Tulipomaliza kufunga, kulikuwa na majaribu na vipindi
vigumu na mara nyingine nalijisikia kuishiwa nguvu, siwezi tena kuendelea na
Bwana. Lakini alinipa nguvu. Nilianza kusikia sauti yake na kumjua vema zaidi.
Tukawa marakifi wazuri. Bwana ni rafiki yetu mwema, na Roho Mtakatifu pia.
Niliwahi mwambia, "Bwana, wewe ni rafiki yangu bora. Nataka kukujua
vema," na nilishirikiana naye katika mawazo yangu yote.
Nilimwomba kipindi chote cha mwezi Agosti hadi Novemba,
na mtumishi wa Bwana akaja nyumbani kwetu na kusema, "Bwana
akubariki." Nikajibu, "Ameni." Kisha akasema, "Nimekuja
kukuletea ujumbe toka kwa Mungu…...Jiandae, kwasababu Bwana atakuonesha mambo makubwa,
magumu usiyoyajua. Atakuonesha wewe Mbinguni na kuzimu kama ulivyokuwa
unamwomba neno la Yeremia 33:3." Nikamwuliza, "Ndiyo, lakini
umepataje kujua? Sijamweleza yeyote." Akanijibu, "Mungu unayemtumikia
na kumsifu, ndiye nimsifuye, alinieleza kila kitu." Mara tukaanza kuomba.
Baadhi akina dada toka kanisani kwetu na wana familia wangu wakaungana nasi
kuomba. Lakini mara tulipoanza kuomba, nilianza kuona Mbingu zikifunguka. Mara
nikasema “naona mbingu zikifunguka, na malaika wawili wanashuka kuja tulipo"
Mtumishi wa Mungu akasema “waulize kwanini wamekuja hapa”
Walikuwa warefu na wazuri wakupendeza; wana mbawa
nzuri. Walikuwa wakubwa na wenye kung’aa, na walionekana wakiangaaza, mng’ao
kama wa dhahabu. Walivaa sandozi za vito vya thamani na walivaa mavazi
matakatifu. "Kwanini mko hapa?" Wakatabasamu na kusema, "Tupo
hapa kwasababu tuna kazi yakufanya….. tupo hapa kwasababu unatakiwa utembelee
Mbinguni na kuzimu na hatutaondoka mpaka yote yatakapo pita." Nikawajibu
“safi sana, lakini mimi natamani kutembelea Mbinguni tu, siyo kuzimu”
Wakatabasamu na kuendelea kuwepo na hawakusema lolote zaidi. Baada ya kumaliza
maombi, niliendelea kuwaona wakiwepo.
Pia nilianza kumwona Roho Mtakatifu; ni rafiki yangu
bora; ni Mtakatifu, amejaa pote na yuko kila mahali wakati wote. Ninamwona,
anaangaza na kung’aa sana, naona tabasamu lake na mtazamo wake wa upendo! Ni
vigumu sana kumwelezea, kwa sababu ni mzuri zaidi ya malaika. Malaika wana
uzuri wao lakini Roho Mtakatifu ni zaidi sana kwa yote. Naweza kuisikia sauti yake, sauti ilijaa upendo na matulizo
makuu. Siwezi kuelezea kabisa sauti yake; kama radi si radi wakati huo huo
yakuvutia. Yeye husema “Niko pamoja nawe” Kwa hiyo nalijitahidi kuendelea
kutembea na Mungu, japo majaribu yalizidi kutuzingira. Tulikuwa tunapita
kipindi kigumu sana, lakini chenye ushindi waajabu. Mie husema “Bwana, mapenzi
yako yatimizwe.” Niliendelea kuwaona malaika wale hata nikiwa shule na pia
darasani. Nilikuwa mwenye furaha ajabu kwa sababu niliwaona vema.
Mtumishi wa Bwana, aliyetutembelea, aliniambia
nijiandae, kwa sababu nitakwenda kuona Mbingu na kuzimu. Lakini pia aliniambia
kitu kigumu. Alisema “Nitakufa.” Haikuwa rahisi niliposikia neno hili.
4
"Nitakufa namna gani? mie mdogo sana",
Nilimuuliza. Akanijibu, “Usihofu juu ya lolote, Kila kitu Mungu afanyacho
hakina makosa wala mawaa, na atakurejesha duniani, ili utoe ushuhuda juu ya
Mbinguni na Kuzimu, kwakuwa hilo ndilo Bwana anataka sote tujue” Nikasema
“Amen, lakini nitagongwa na gari au nitakufaje?” Mawazo yalinisonga sana,
lakini Bwana akaniambia nisihofu, kila kitu kiko katika uwezo wake. Nikasema,
“Ahsante Bwana”
Ilipofika tarehe 6 Novemba, baada ya kurejea nyumbani
toka shule, malaika wale walikuwa nami, hata nilipokuwa namsifu Bwana. Wao
walikuwa hawaongei nami; bali walidumu kusema, “Mtakatifu, Mtakatifu,
Mtakatifu, Hallelujah," huku wakimpa utukufu, heshima na sifa Baba wa
Mbinguni. Roho Mtakatifu pia alikuwa na malaika wale huku akifurahi. Watu wengi
husema injili/ wokovu ni wa kuchosha/kukera, lakini huo ni uongo mkubwa toka
kwa mwovu ili kuwafanya watu wasitafute uwepo wa Mungu. Nami pia niliamini
hivyo hapo kwanza, lakini baada ya kukutana na Bwana na Roho Mtakatifu, najua
injili haikeri wala kuchosha, niburudisho la ajabu hapa duniani!
Ninaweza kumwona; kucheza na kuongea naye Roho
Mtakatifu. Lakini malaika walikuwa hawaongei nami, ila walikuwa wakimsifu
Bwana. Nikimwambia Roho twende nami nakufanya hili na lile huja na kuwa nami.
Ninaweza kujihisi na kumwona vema. Japokuwa wengi hawamwoni, yeye yupo!
Mahusiano haya yamendelea, hata hakuna sababu ya kuyasimamisha, hasa baada ya
kuonja radha yake na faida za Roho Mtakatifu…… hakuna njia ya kujitenga naye
jinsi alivyo mwema na wafaida, hasa nikikumbuka alikonitoa, jinsi nilivyokuwa,
ninamshukuru sana kwa rehema zake na upendo wake kwa wanadamu na kwangu mimi!
Tarehe 7, Novemba, nilipokuwa narudi nyumbani,
nikasikia sauti ikisema “Jiandae, kwakuwa leo utakufa,” Nilijua kuwa ni Roho
Mtakatifu kwa vile nilimwona vema. Niliipuuza sauti yake na kusema “Bwana,
Sitaki kufa leo!” Lakini alirudia, “Jiandae, kwakuwa leo utakufa!” Mara hii
sauti ilikuwa ya juu zaidi na mkazo mkubwa. Nikajibu, “Bwana, najua ni wewe
unayesema nami; nimeuliza ili kupata uhakika tu, mapenzi yako yatendeke.
Nitafanya kila utakalo niambia, najiachia kwako Bwana, japo naogopa, najua upo
nami, nawe ni wa kweli.” Niliomba, “Bwana, Yule mtumishi wako uliyemtumia
kunipa ujumbe mara ya kwanza, mlete muda huu, nimkute nyumbani, na umpe tena
neno hili aseme nami kuwa leo ndiyo siku yangu ya kufa.” Sasa mara zote Bwana hujua
ya nyuma, yaliyopo na yajayo. Alijua kuwa nitamwomba neno hili. Kwa hiyo
nilipofika nyumbani nikamkuta mtumishi wa Bwana ameishafika!.
Maxima (Mama ya Binti): Binti yangu alipofika nyumbani,
tulikuwa jikoni. Mara Angelica alipomwona mtumishi wa Bwana, akasema, “Bwana
akubariki.” Mtumishi wa Mungu akajibu, “Bwana akubariki nawe. Je uko tayari?
Kwa kuwa leo ndiyo siku Bwana atakayo kuchukua, saa kumi jioni.” Angelica
alisimama na kushikwa na mshangao kwamba Bwana amejibu ombi lake na kufanya
vilevile alivyomwomba njiani.
Angelica: Niliposikia hayo maneno ya mtumishi,
nikasema, “Ameni... lakini sitaki kufa, sitakufa! Hapana, Bwana, naogopa,
naogopa sana, ninahofu kubwa!” Mtumishi wa Bwana akasema, “Tuombe ili hofu
ikutoke sasa kwa jina la Bwana.” Nikasema, "Ameni" na tukaomba.
Ghafla nikajisia hofu yote imenitoka na furaha isiyoelezeka ikajaa ndani
mwangu, nakuanza kuwaza kuwa kifo ni kitu chema kuliko vyote nikitamanicho
kinifike! Nikanza kutabasamu na kicheka wakati huo kila mmoja
5
aliyepo akinitazama. Wakaniona jinsi nilivyobadilika
toka unyonge na kuwa mwenye furaha. Nilikuwa natabasamu, narukaruka na kuimba.
Picha wakimwombea:
Maxima: Binti yangu ghafla akawa mwenye furaha ndani ya
moyo na kuanza kula. Alionja karibia kila kitu kilichokuwepo, huku akisema,
“Kama sitarudi, sawa nimeshakula na kushiba.”
Angelica: Kila mmoja akaanza kucheka na kuuliza,
“kwanini uko hivyo badala ya kuwa na huzuni, unafuraha na mwenye raha?”
nikawajibu, “Ndiyo ninafuraha: ninakwenda kumwona Bwana, nitakuwa naye, lakini
sijui kama nitarudi. Kwa hiyo nataka kugawa vitu vyangu vyote.” Wote
wakastaajabu na kuniuliza, “Unataka kugawa vitu vyako vyote?” macho ya mama
yangu yalinitazama kwa mshangao zaidi!
Maxima: Binti yangu akaanza kugawa vitu vyake. Aligawa
vyote, vyote! Ma-dada wa kanisani walikuwepo, nao pia aliwapa baadhi ya vitu
kwa kila mmoja. Nilipomuuliza nia yake, alisema, “Kama nikirudi, watanirejeshea
vyote, lakini nisiporudi, watabaki navyo.”
Angelica: Niliwaza huzuni aliyokuwa nayo mama yangu
niliposema maneno hayo. Lakini nilijisikia furaha tupu, kwa hiyo nikaendelea
kugawa vitu: nguo, kitanda, simu ya mkononi, kila kitu, lakini kwa sharti: kama
nikirudi, kila kitu kitarejeshwa kwangu. Wote wakaanza kucheka.
Maxima: Binti yangu alikuwa na msimamo na nia ya dhati,
lakini kama mama nilishikwa na huzuni sana. Haikuwa jambo rahisi. Niliwaza,
“Bwana muda huo ukiwadia, itakuwajekuwaje?” Sikuweza kuelewa. Na walipoanza
kuomba, nilikuwa napanga vitu ndani ya nyumba. Walisema, “Dada njoo tuombe.”
Lakini niliwajibu, “Nyie endeleeni, nitajiunga nanyi muda si mrefu. Ngoja
nimalizie kazi hii.”
Angelica: Wote walikuwa wananiangalia mimi tulipokuwa
tunaomba. Niliomba, “Bwana, nataka kufanya mapenzi yako. Wewe si mwanadamu hata
useme uwongo au ujute, najua wewe ni mkweli. Kama nitakuaibisha, basi vema
unichukue moja kwa moja; lakini kama nitayafanya mapenzi, basi unirejeshe tena,
lakini nisaidie kusema ukweli, niandae mimi, nisaidie kuhubiri na kuwaambia
watu kutubu.” Hiyo ndiyo ilikuwa sala yangu fupi sana. Nilimwambia mtumishi wa
Bwana,
6
“Usimwambie mama yangu maneno niliyomwomba Bwana.” Naye
akajibu, “sitamwambia sasa, lakini mara Bwana atakapokutwa, nitamwambia.”
Tuliendelea kuomba na kuungana katika duara. Maxima: Ilipofika saa 9:30 jioni,
Bwana akamwambia mtumishi wake ampake mafuta binti yangu. Kwa hiyo baadhi yetu
tulikwenda chumbani na kumpaka mafuta. Alitupa dakika mbili tumpake mwili
mzima, toka kichwani hadi chini, kila mahali, mwili mzima. Akawa mwili wote
amepakwa mafuta.
KIFO CHAKE Angelica: Mama yangu na dada mmoja, Fátima
Navarrete, walinipaka mafuta. Kadri walivyokuwa wananipaka, nilijisikia kama
kuna kitu kinanifunika, kama kioo kilinizunguka mimi. Ni vigumu kuelezea,
nilijisikia kama nimezingirwa na ngao fulani, na nashindwa kuelezea nilivyokuwa
najisikia. Baada ya hapo kila walipojaribu kunigusa walishindwa!
Maxima: Kadri tulivyokuwa tukimwombea Angelica,
nilijaribu kuweka mkono juu yake, nilishindwa! Alikuwa amezingirwa na kitu.
Ilikuwa ajabu, hakuna aliyeweza kumgusa tena! Uzio huo ulianzia kichwani hadi
miguuni, karibia sentimenta 30 (Inchi 12). Hilo lilinitisha zaidi mimi.
Nimewawekea mikono wengi kabla, katika huduma ya Bwana, lakini jambo kama hili
halijawahi kutokea! Nikasema, “Oh, kuna jambo lazima linatendeka,” na nikaanza
kuomba na kumshukuru Bwana. Ghafla, nikasikia furaha kubwa sana. Huzuni
iliyokuwa moyoni ikanitoka, maumivu yakakoma na sasa nikasikia raha na furaha
ajabu! Tuliendelea kuomba na ilipofika saa 10.00 jioni, binti yangu akaanguka
sakafuni.
Angelica: Wakati wa maombi, nilisikia kuishiwa pumzi;
nikashindwa kupumua. Nikasikia maumivu tumboni na moyoni. Nilijisiki damu
ikisimama, na ghafla maumivu makali mwili mzima. Nililoweza kusema, “Bwana,
nipe nguvu, nipe mimi nguvu!” kwasababu nilijisikia kushindwa kuendelea zaidi.
Sikuwa na nguvu kabisa, zote zilinitoka! Na nilipoangalia juu mbinguni, katika
roho, si kwa macho ya mwilini, niliona mbingu zikifunguka. Niliwaona malaika,
siyo wawili au kumi, bali kwa mamilioni wakiwa pamoja wamekusanyika. Katikati
yao niliona mwanga, mara 10,000 zaidi ya jua. Na nikasema, “Bwana ni wewe
unayekuja!”
Maxima: Alipoanguka chini, tulijaribu kumsimamisha,
lakini hakuweza kusimama mwenyewe. Muda huu tuliweza kumgusa. Alikuwa akisema,
“Omba. Sina nguvu, mama, sina nguvu na ninasikia maumivu.” Mwanzo alisikia
maumivu tumboni, na baadaye moyoni. Tuliendelea kuomba na kumsihi Bwana. Bwana
alichukua maisha yake! Picha Mwili wake:
7
Sijawahi katika maisha yangu kumwona mtu akifa.
Nilishuhudia binti yangu, akigugumia maumivu! Haikuwa rahisi hata kidogo!
Sikuweza kuelewa maneno yake ya mwisho, na mwisho alitulia. Niliweka mikono
yangu usoni pake, na kioo mdomoni kuona kama alikuwa anapumua. Hakuwa na pumzi
tena, alitulia kimya kabisa. Nilimshika, alikuwa angali na joto kama kawaida.
Nilichukua shuka na kumfunika na kwa muda mfupi akaanza kupoa na kuwa wa baridi
sana. Nywele zake zikalala, kama za maiti na akabadilika ubaridi wa barafu.
Angelica: Yesu alikuwa anashuka chini, na nikajisikia
mwili ukifa. Kadri Yesu na malaika walivyozidi kukaribia, nikajisikia kuondoka,
na sikuwa mimi tena. Sikuwa hai tena, nilikuwa nakufa na kugugumia maumivu!
Wakati mwili wangu ulipoanguka chini, walikuwa tayari wamefika. Nyumba yetu
ilijaa malaika, na katikati yao niliona mwanga mkali kuliko wa jua! Ilikuwa
vigumu; nilisikia maumivu makali wakati roho yangu ilipotenganishwa na mwili.
Nilikuwa nalia na kupiga kelele, kadri nilivyoona mwili wangu sakafuni.
Nilimuuliza, “Bwana, nini kinachotokea? Nini kinachotokea?” Nilijaribu kuugusa
mwili wangu na kuurudia tena, lakini nilipojaribu, ilikuwa kama kushika hewa:
sikuweza kuugusa, mkono wangu ulipitiliza. Hakuna kati ya waliokuwa wananiombea
aliyenisikia! Na nikapiga kelele, “Bwana, nisaidie mimi!” Maxima: Mume wangu alifika tulipokuwa tunaomba, na alimkuta pale.
Bwana alinipa nguvu kwa kuwa sikujua la kufanya. Ilikuwa kama vile yuko
mahututi (kwenye coma), lakini nilijua yuko salama, kwasababu ilikuwa ni kazi
ya Bwana. Kwahiyo nikasema “Bwana, mapenzi yako yafanyike.”
BWANA YESU KRISTO Angelica: Wakati huo nasikia sauti ya
Bwana, sauti nzuri kama radi lakini ya UPENDO, “Usiogope, Binti, kwa kuwa mimi
ni Yehova, Mungu wako, na nimekuja hapa kukuonesha niliyokuahidi wewe. Inuka,
kwa kuwa mimi ni Yehova, ninayekushika mkono wako wa kuume na kukuambia, usiogope,
nitakusaidia wewe." Ghafla, nikasimama. Nilikuwa nimepiga magoti chini,
ninauangalia mwili wangu, nikitaka kuurejea bila mafanikio. Niliposikia sauti
yake, woga ukanitoka, na sikuwa na hofu tena. Nilipoanza kutembea, malaika
wakaanza kufungua njia. Kulikuwa na mwanga mkali ung’aao, na nilipouangalia
nilisikia amani ya ajabu. Kadri nilivyoangalia, nilimwona mwanaume mzuri,
mrefu, aliyevaa vizuri na kuvutia sana kumwangalia, mwenye siha njema. Mwanga
ulitoka kwake. Kulikuwa na mwanga mkali kiasi cha kushindwa kumwangalia uso
wake! Lakini niliweza kuona nywele zake za dhahabu ing’aayo na vazi jeupe na
mshipi kifuani pake. Ukisomeka, “MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.”
Nilimwangalia miguuni pake, alikuwa amevaa sandozi
zenye mng’ao wa dhahabu, dhahabu safi. Alikuwa mzuri sana! Akaninyooshea mkono
wake. Nilipomshika mkono wake, haikuwa kama nilipojaribu kuugusa mwili wangu,
mkono haukupitiliza. Nikauliza, “Nini kinachotokea?” naye akasema,
“Nitakuonesha wewe kuzimu ili ukirudi uwaambie wanadamu kuwa kuzimu ni halisi;
kuwa ni kweli ipo. Na pia utukufu wangu nitakuonesha wewe, ili uwaambie watu
wangu wajiaandae, kwa kuwa utukufu wangu ni halisi na mimi pia.” Akasema,
"Binti, usiogope” akarudia kusema tena na mimi nikasema, "Bwana,
nataka tu kwenda Mbinguni, lakini siyo kuzimu, kwasababu nimesikia kunatisha!”
Akasema, “Binti, nitakuwa nawe. Sitakuacha huko na nitakuonesha huko mahali
kwasababu wengi wanajua kuzimu ipo lakini hawaiogopi.
8
Wanaamini ni mchezo, na kuzimu ni mzaha, na wengi
hawajui lolote juu yake. Ndiyo maana nitakuonesha wewe huko kwa sababu
wanaopotea ni wengi kuliko wanaoingia katika utukufu wangu.” Aliposema hayo,
niliona machozi yakitiririka kwenye vazi lake. Nikamwuuliza, “Bwana, kwanini
unalia?” Akanijibu, “Binti, kwasababu wengi wanaangamia, na nitakuonesha hii,
ili uende na uwaambie ukweli na wewe usirudie hapo.”
KUZIMU Ghafla, alivyokuwa anaongea, kila kitu kikaanza
kutembea. Ardhi ilitikisika na kupasuka, na nikaona shimo jeusi tii chini.
Shimo:
Tulikuwa tumesimama kama kwenye mwamba na malaika
wakituzunguka. Nikasema, “Bwana, sitaki kwenda mahali huko!” akasema, “Binti,
usiogope niko pamoja nawe.” Kwa sekunde chache tukashuka kwenye shimo jeusi.
Nilijaribu kuangalia lakini kulikuwa na kiza kikuu. Niliona duara kubwa, na kusikia
mamilioni ya sauti.
Nilipata moto. Nikajisikia ngozi yangu kuungua.
Nikamuuliza, “Bwana, hiki ni nini? sitaki kwenda mahali huko!” Bwana akasema
hilo ni lango tu la kwenda kuzimu. Kulikuwa kuna harufu mbaya, yakutisha,
isiyovumilika, na nikamsihi Yesu asinipeleke mimi. Naye akajibu, “Binti, ni
muhimu ufike na kujua sehemu hii.” Nikalia, “Lakini kwanini, Bwana, kwanini?”
naye akasema, “Ili ukawaambie ukweli wanadamu; wanadamu wanaangamia, wanapotea
na wachache sana wanaoingia ufalme wangu.” (Mat.7:14) Akishasema hivi, hulia
sana. Maneno yake yalinitia nguvu na kunihimiza, kwa hiyo nikaendelea kutembea.
Ziwa la Moto:
9
Tulifika mwisho wa tanuru/lango, nilipoangalia chini
niliona umati umefunikwa na miali ya moto. Bwana akasema “Binti, nakupa hii.”
Ilikuwa ni faili kubwa lenye karatasi ambazo hazijaandikwa chochote. “Binti,
chukua na kalamu hii ili uweze kuandika yote nitakayokuonesha, utakayoyaona na
kusikia. Utaandika kila kitu ukionacho na utaishi nayo.” Nikasema, “Bwana,
nitafanya, lakini nimeshaanza kuona mengi mno, Bwana. Ninaona roho zikiteswa,
na kuzamishwa kwenye moto.”
Maxima: Muda uliendelea kupita, na binti yangu alikuwa
bado kalala pale. “Bwana, nini kinachotokea?” Machozi yalikuwa yakimtoka kwenye
macho, lakini kila nilipomfuta, yalitoka tena. Nikaweka kioo mdomoni pake kuona
kama anapumua, hakukuwa na pumzi. Tuliangalia mapigo ya damu, wapi, hakuna
kitu!. Tuliweka mikono tumboni pake, wapi! Hakuna kitu. Mtumishi wa Bwana
akasema, “mahali alipo sasa, siyo mahali pa kutabasamu bali mahali pa mateso.”
Angelica: Nikamwambia Yesu, Nitashuhudia kuwa kuzimu ni
halisi, kwamba ipo, lakini nitoe hapa sasa!” na akanijibu, “Binti, hatuja ingia
bado mahali penyewe, na sijakuonesha chochote, tayari unataka nikutoe huku?”
nikasema “Bwana, tafadhari nitoe mahali hapa,” tukaendelea kushuka kwenye
korongo/shimo lakutisha! Nikaanza kulia na kupiga yowee, “Bwana, hapana,
hapana, hapana, hapana……… Sitaki kwenda!” naye hujibu, “Unatakiwa kuona haya.”
Niliona mapepo yakutisha, ya kila aina, makubwa na
madogo. Yalikuwa yanakimbia sana, na yameshika vitu mkononi. “Bwana, kwanini
yanakimbia hivyo na yameshika nini?” akanijibu, “Binti, wanakimbia hivyo
kwasababu wajua muda wao karibu kwisha, kwasababu muda wa kuwaharibu/kuwapoteza
wanadamu, hususani watu wangu. Na walivyoshika mkononi ni mishale ya kuwaharibu
wanadamu, kwasababu kila pepo amepewa jina na kwa kadri ya jina lake, ana
mishale ya kumharibu mtu na kumleta huku kuzimu; malengo yao ni kumharibu mtu
na kumleta kuzimu.” Na niliendelea kuona mapepo yakikimbia na kutoka kuelekea
duniani na Bwana akaniambia; “Wanakwenda duniani ili kuleta na kuwatupa
wanadamu huku." Alipokuwa akisema hivyo, Bwana hulia, hulia sana. Kila
alipolia nami nililia pia.
Maxima: Binti yangu alikuwa amekufa kwa masaa 23,
lakini sikutoa taarifa kwenye mamlaka yoyote. Niliomba, “Bwana, nitasubiri kwa
masaa 24. Kama binti yangu hatarudi ndani ya saa 24, nitampigia simu Daktari.”
Lakini, Bwana alimrejesha kabla ya saa 24 hazijatimia.
Angelica: Bwana akaniambia, “je uko tayari kuona
nitakachokuonesha wewe?” Nikasema, “Ndiyo Bwana,”. Alinipeleka kwenye sero
moja, ambapo nilimwona kijana akiwa matesoni katikati ya miali ya moto.
Nikajulishwa namba sero yake, japokuwa sikuweza kujua ile namba, ilionekana
kama imeandikwa kinyume hivi. Palikuwa na nembo kubwa mle ndani, na kijana
alikuwa na namba 666 kwenye kipaji cha uso. Pia alikuwa na aina ya kipande cha
chuma imebandikwa kwenye ngozi yake. Funza walikuwa wanamtafuna, haikuweza
kuharibu kipande kile; wala moto haukuweza kukiunguza. Akapiga kelele, “Bwana,
nirehemu mimi. Nitoe mahali hapa. Nisamehe mimi Bwana!” lakini Yesu alimjibu,
“umechelewa, umechelewa sana: nilikupa fursa lakini hutaka kutubu.” Nikamuuliza
Yesu, “Bwana, kwanini huyu yuko hapa?” mara nikajulishwa.
10
Akiwa duniani, kijana huyu alijua neno la Mungu, lakini
ghafla akajitenga na Bwana na kuchagua pombe, madawa ya kulevya na kupita
katika njia zisizofaa. Hakutaka kufuata njia ya Bwana. Yesu alimwonya mara
nyingi juu la litakalompata. Yesu akasema, “Binti, yuko hapa kwasababu kila anayeyakataa
maneno yangu, anaye amhukumuye: lile neno nilisema naye litamhukumu siku ya
mwisho,” (Yohana 12:48) na Yesu akalia tena.
Bwana akilia, nitofauti nasi tuliavyo na zaidi yetu.
Yeye hulia na maumivu makali moyoni na uchungu usioelezeka. Bwana akasema,
"Sikutengeneza kuzimu kwaajili ya wanadamu,” Nikamuuliza, “Sasa Bwana
kwanini wanadamu wapo huku,” Akanijibu, “Binti, niliumba kwajili ya shetani na
malaika zake, ambayo ni mapepo;(Mat. 25:41) lakini, kwasababu ya dhambi na
kukosekana kwa toba, wanadamu huishia hapa, na wengi wangamiao kuliko wanaofika
katika utukufu wangu!" Akaendelea kulia na huniumiza sana nimwonapo
akilia. "Binti, nalitoa maisha kwaajili ya wanadamu, ili wasiangamie, ili
wasiishie hapa [Kuzimu]. Nalitoa maisha yangu kwa upendo na huruma, ili
wanadamu waendee toba na kuingia katika ufalme wa Mbinguni.” Yesu kwa huzuni
huugua kiasi cha kushindwa kustahimili maumivu, kadri aonavyo watu pale kuzimu.
Kwa kuwa na Yesu, kulinifanya nijisikie salama.
Niliwaza, “kama nikimwacha Bwana aende, ninge-nasa kuzimu pale” Nikamuuliza,
“Yesu, je nina ndugu yangu mahali hapa?” Akanitazama kwa jinsi nilivyokuwa
nalia na akasema, “Binti, niko nawe,” Kwasababu nilikuwa mwenye hofu sana.
Akanipeleke kwenye sero nyingine. Sikuwahi kuwaza kumwona ndugu yangu kwenye
sero ile. Nilimwona mwanamke akiteswa, alikuwa na funza wakimla uso wake, na
mapepo yakimchoma mikuki mwilini. Naye hupiga kelele, “Hapana, Bwana,
nihurumie, nisamehe mimi, tafadhari, nitoe mahali hapa kwa dakika moja!” (Luka
16:24)
Kuzimu, watu huteswa na kumbukumbu za waliyoyafanya
duniani. Mapepo hudhihaki watu na kuwaambia, “abudu na kusifu kwasababu huu
ndiyo ufalme wenu!” na watu hupiga kelele
11
wakikumbuka kuwa walimjua Mungu, kwasababu walijua
neno. Walimjua Bwana waliteswa mara dufu ya wengine.
Bwana akasema, “Hakuna tena nafasi kwa walioko
pale[kuzimu]; kungali na nafasi kwa walio hai.” Nikamuuliza, “Bwana, kwanini
bibi yangu mkubwa yupo pale? Sijui kama alikujua wewe. Kwanini yupo kuzimu
Bwana?” akanijibu, “Binti, yupo hapa kwasababu alishindwa kusamehe….. binti,
yeyote asiyesamehe, sitamsamehe huyu.”
Nikamuuliza, “Bwana, lakini wewe husamehe, na una
rehema.” Naye akanijibu, “Ndiyo, binti, lakini nilazima kusamehe, kwasababu
hawajawasamehe wengi, na ndiyo maana wengi wapo hapa, wameshindwa kusamehe……
nenda kawaambia wanadamu ni muda wa kusamehe, hasa hasa watu wangu, kwakuwa
wengi miongoni mwa watu wangu hawajasamehe. Waambie waache malaaumu, mafundo,
chuki mioyoni mwao, kwa kuwa ni muda wa kusamehe! Kama kifo kikimsitukiza mtu
aliyeshindwa kusamehe, huyo mtu atakwenda kuzimu, kwakuwa hakuna awezaye
kununua maisha.” Tulipoondoka hapo, bibi yangu mkubwa alifunikwa na moto na
akapiga makelele, "Aaaah," na akaanza kutukana jina la Mungu, na
kumlaani Bwana; kila mtu kuzimu humtukana Mungu.
Tulipoondoka eneo lile, nikaona kuwa kuzimu imejaa roho
ziteswazo. Watu wengi huinua mikono nje, wakimwomba Yesu msaada wa kuwatoa nje.
Lakini Bwana hakuwa na lolote la kufanya kwao, nao huanza kumtukana Mungu. Mara
Yesu hulia sana na kusema, “Inaniumiza sana kuwasikia, inaniumiza mimi sana
wanavyofanya, kwasababu siwezi kufanya lolote kwaajili yao. Ninacho kueleza ni
hiki; nina nafasi kwa hao walioko duniani, ambao hawaajafa, walio hai, wanao
muda wa kutubu!”
Bwana akaniambia kuna watu wengi maaruku huku kuzimu,
na pia wengi waliomjua Bwana. Akasema, “Nitakuonesha upande mwingine wa
tanuru.” Tukaenda mahali penye mwanamke aliyezingirwa na miali ya moto. Alikuwa
katika maumivu makubwa na kupiga makelele, akiomba huruma kwa Bwana. Yesu
akanyoosha mkono kwake na akaniambia, “Binti, Yule mwanamke umwonaye pale,
amezingirwa na miali ya moto ni Selena.” Kadri tulivyokuwa tunamkaribia,
akapiga kelele, “Bwana, nihurumie mimi, nisamehe mimi Bwana, nitoe mahali
hapa!” lakini Bwana akamtazama na kusema, "Umechelewa, umechelewa sana,
huwezi kutubu sasa.” Selena
Aliponiona mimi akasema, “Tafadhari, nakuomba wewe,
waambie watu hivi, tafadhari sema na usinyamaze; nenda waambie wasije mahali
hapa; nenda waambie wasisikilize nyimbo zangu, wala wasiimbe hizo nyimbo.”(1
Yohana 2:15) Nikamuuliza, "kwanini unataka mimi niwaambie hivyo?"
12
naye akanijibu, "Kwasababu kila wakati watu
wanaposikiliza nyimbo zangu, nateswa zaidi na zaidi, na mtu anayeimba na
kusikiliza nyimbo zangu, anaelekea mahali hapa. Tafadhari, nenda uwaambie
wasije huku; nenda waambie kuzimu ni halisi, ipo kweli!”. Akapiga kelele na
mapepo humchoma mikuki na Selena kulia, “Nisaidie mimi, nihurumie mimi Bwana!”
lakini kwa huzuni Bwana alimwambia, “umechelewa sana.”
Nikaangalia pande zote za eneo lile, lilikuwa limejaa
waimbaji na wasanii waliokufa. Walikuwa wakiimba na kuimba, bila kusimama.
Bwana akanifafanulia, “Binti, mtu aliyepo hapa, lazima aendelee kufanya kile
alichokuwa anafanya duniani, kama hajatubu."
Kadri nilivyokuwa naangalia eneo lile, niliona mapepo
mengi yakinyunyiza vitu kama mvua. Nilidhani ni mvua inanyesha. Lakini niliona
watu kwenye miali ya moto wakikimbia mbali na ile mvua na kupiga yowee,
“Hapana, nisaidie, Bwana!..... Hapana, haiwezekani kuwa hivyo,” na mapepo
yalikuwa yanacheka na kuwaambia watu, “Sifu na kuabudu kwasababu hapa ni ufalme
wenu milele na milele!” Niliona miali ya moto ikiongezeka na funza za watu
zikiongezeka zaidi! Hayakuwa maji yale bali kiberiti cha kuongeza miali ya moto
na kuongea maumivu ya kila mtu. Nikamuuliza Yesu, “Ni nini kinachotokea?.....
Bwana, ni nini hiki?” Bwana akanijibu, “Huu ni ujira wa yeyote asiyetubu.”
(Zaburi 11:6).
Bwana akanipeleka mahali alipo mtu aliyejulikana sana.
Kabla ya maono haya, nilishi maisha kama msichana wa kikristo wa nia mbili. Nilidhani
kila mtu anayekufa anakwenda Mbinguni; wale walifanyiwa ibada za mazishi
watakwenda mbinguni, kumbe sikuwa sahihi, nilikosa. Alipofariki Papa John Paul
II, marafiki zangu na ndugu walisema amekwenda mbinguni. Taarifa zote kwenye
LUNINGA [TV], na vyombo mbalimbali vya habari vilisema, "Papa John Paul II
amefariki, apumzike kwa amani. Anafurahia sasa kuwa na Bwana na malaika
Mbinguni" na mimi niliamini yote kuwa ndivyo. Lakini kumbe nilikuwa
najidanganya mwenyewe, kwasababu nimemwona kuzimu, akiteswa kwa miali ya moto.
Nilimtazama uso wake, alikuwa mwenyewe Papa John Paul II! Bwana akaniambia,
“Angalia, Binti, Yule mwanaume umwonaye pale, ni Papa John Paul II. Yuko hapa;
akiteswa kwasababu hakutubu.” Papa John Paul II
Lakini nikamuuliza, “Bwana, kwanini yuko hapa? Alikuwa
akihubiri kanisani.” Yesu akanijibu, “Binti, hakuna mwasherati, wala muabudu
sanamu, hakuna mchoyo na hakuna mwongo atakayerithi ufalme wangu.” (Eph 5:5)
Nikamjibu, “Ndiyo, najua ni kweli, lakini nataka kujua kwanini yuko hapa, kwasababu
alikuwa akiwahubiria umati wa watu!" Na Yesu akanijibu, “Ndiyo, Binti,
alisema mengi, lakini hakusema kweli kama ilivyo. Hakusema kweli na kweli
aliijua na japokuwa aliijua kweli, alipenda fedha zaidi ya kuhubiri habari za
wokovu. Hakutoa uhalisia; hakusema kuzimu ni halisi na mbinguni kupo; Binti,
sasa yuko mahali hapa."
13
Nilipomwangalia mtu huyu, alikuwa na joka kubwa lenye
sindano nyingi mwilini mwake, limemzingira shingoni, naye hujaribu kumtoa.
Nalimwomba Yesu, “Bwana, msaidie!” Mwanaume hupiga kelele, “Nisaidie mimi,
Bwana nihurumie; nitoe mahali hapa; nisamehe mimi! Ninatubu Bwana; Nataka
nirudi duniani, nataka nirudi duniani nikatubu.” Bwana alimtazama na kumwambia,
“Ulijua vizuri yote haya. Ulijua vema kuwa kuzimu ni halisi, ipo…….. umechelewa;
hakuna tena nafasi kwaajili yako.”
Bwana akasema, “Tazama Binti, nitakonesha maisha ya mtu
huyu.” Yesu akanionesha kioo kikubwa kama LUNINGA [TV]; nikaona alivyotoa misa
mara nyingi kwa umati wa watu. Na watu wale walivyokuwa waabudu sanamu. Yesu
akasema, “Tazama, Binti, wapo waabudu sanamu wengi hapa [Kuzimu]. Ibada ya
sanamu haiwezi kuokoa Binti. Ni mimi pekee niwezaye kuokoa, na nje yangu hakuna
mwingine aokoaye. Nawapenda wenye dhambi, lakini nachukia dhambi Binti. Nenda
na uwaambie wanadamu kuwa nawapenda na ninataka waje kwangu.” Kadri Bwana
alivyokuwa akisema, nilianza kuona mtu huyu akipokea makusanyo makubwa ya
sarafu na fedha; vyote alivihifadhi. Alikuwa na fedha nyingi sana. Naliona sura
yake imeketi katika mamlaka yake, lakini pia naliweza kuona zaidi. Japo ni
kweli watu hawa hawaoi, ninakuhakikishia wewe, sizushi, Bwana alinionesha mimi,
wanalala na masista; na wanawake wengi! Bwana akanionesha watu hawa wanaishi
kwa uasherati, na neno linasema hakuna mwasherati atakayerithi ufalme wake. Kadri
nilivyokuwa naona, Bwana akaniambia, “Tazama, Binti, yote ninayokuonesha, ndiyo
yanayoendelea, ndivyo alivyoishi [Papa] na ndivyo yanayotokea katikati ya watu
wengi, katikati ya mapadre na mapapa waliopo.” Kisha Bwana akasema, “Binti,
nenda na uwaambie wanadamu ni muda wa kugeukia.”
Bwana akanionesha sehemu watu wengi wanavyoelekea
kuzimu. Nikamuuliza, “Bwana, namna gani wanakuja huku?” akanijibu,
“Nitakuonesha.” Akanionesha lango lenye watu wengi wakipita. Watu hawa walikuwa
wamefungwa toka mikononi hadi miguuni. Walivaa mavazi meusi na kubeba mizigo
mgongoni mwao. Yesu akasema, “Binti, hao watu uwaonao hawanijui mimi bado.
Mizigo waliyobeba ni dhambi, lakini nenda waambie walete mizigo kwangu, nami
nitawapumzisha; kwa kuwa mie ndiye mwenye kusamehe dhambi zao zote…. Binti,
nenda na uwaambie waje kwangu, kwani nawasubiri na mikono yangu iko wazi
kuwapokea, na uwaambie hapo wanaelekea mahali hapa [kuzimu].”
Kadri nilivyokuwa nawatazama watu wakitembea,
nikamwambia, “Bwana, Yule mtu pale ni binamu yangu; na Yule kijana pia, Bwana,
na Yule binti pale anayelekea kuzimu; oh familia yangu inakuja huku kuzimu!”
Bwana akajibu, “Binti, wanakuja huku, lakini nenda uwaeleze wanakoelekea, nenda
waeleze kuwa wanakwenda kuzimu. Nenda waeleze kuwa nimekuchagua wewe uwe mlinzi
wangu…… nimekuchagua wewe kama mlinzi, hii inamaanisha kuwa unatakiwa uwaambie
ukweli. Unatakiwa uende uwaeleze yote niliyokuonesha wewe. Kama hutawaambia na
jambo likampata mtu huyu, damu yake itakuwa juu yako, lakini ukiende na kufanya
nilivyokueleza, hapo mtu huyu nitamdai mwenyewe. Kama mtu hatatubu, hapo wajibu
ulionao utaondolewa, kwa kuwa atadaiwa mwenyewe na damu yake haitakuwa juu
yako. (Ezekia 3:18)"
Yesu akaniambia wengi wa watu maarufu wanaelekea huku
[kuzimu], maarufu na watu muhimu. Kwa mfano, Michael Jackson. Huyu alikuwa
maarufu duaniani kote lakini alikuwa mjumbe wa
14
shetani. Japokuwa wengi wanaweza wasione na kuelewa
hivyo, lakini huo ndiyo ukweli. Huyu alikuwa na mkataba na shetani:
alikubaliana na shetani ili awe na heshima na sifa ilikuwa vutia wapenzi wengi.
Michael_Jackson
Hizo hatua na mitindo aliyokuwa anafanya, ndivyo
nilivyoona mimi mapepo yakicheza na kutembea yanapotesa watu kuzimu. Yalikuwa
yanateleza kwa kurudi nyuma na siyo mbele, huku yakipiga kelele; yakifurahia
mateso wanayopata watu. Ngoja nikuambia wewe kuwa Michael Jackson yuko kuzimu.
Bwana alinionesha baada ya kufa Michael. Alinionesha Michael Jackson akiteswa kwenye
miali ya moto. Nikalia kwa Yesu, “Kwanini?” haikuwa rahisi kuona mtu huyu
alivyokuwa anateswa na alivyokuwa analia na kupiga mayowe. Yeyote anayesikiliza
nyimbo za Michael Jackson au kuziimba au ni mpenzi/shabiki wa Michael Jackson,
ninakuonya kuwa shetani anakutega katika mtego wake ili mwisho uishie kuzimu.
Mara hii, jitoe na kumkana shetani kwa jina Yesu! Yesu anataka kukuweka huru
wewe, ili usipotee milele. Bwana akaniambia, “Binti, kuna watu wanijuao pia
wanakuja huku.” Nikamuuliza, “Bwana, inakuwa je mtu akujue harafu aje huku?”
akanijibu, “Mtu Yule aliyeacha njia zangu na mtu Yule anayeishi aina mbili za
maisha [wokovu na dhambi].” Akaanza kunionesha watu wanaoelekea kuzimu.
Walikuwa wamefungwa kamba toka mikononi hadi miguuni. Kila mmoja alivaa vazi
jeupe, lakini limetobokatoboka, lina-mabakamabaka na limekunjamana. Yesu
akaniambia, “Binti, angalia watu walioniacha mimi. Binti, nataka kukueleza,
siji duniani kwaajili ya watu hawa. Nakuja kwaajili ya watakatifu, waliotayari,
wasiolaumiwa, wasio na makunyanzi na wasio na mawaa…… nenda uwaambie warejee
kwenye njia zao za zamani,” (Efeso 5:26-27) Nilianza kuwaona wengi miongoni mwa
wajomba zangu na watu wengine wengi waliorudi nyuma na kuziacha njia za Bwana.
“Nenda kawaambie ninawasubiri, walete mizigo yao nami nitawapumzisha."
YESU alikuwa analia baada ya kusema hayo, “Binti, wanakuja huku [kuzimu]. Nenda
kawaambie wajomba zako; nenda kawambie ndugu zako kuwa wakuja huku! Binti,
wengi hawatakuamini, lakini mimi ni shahidi wako mwaminifu, ni shahidi wako
mwaminifu. Sitakuacha wewe. Hata kama hawataamini, Binti, nenda na uwaambie
ukweli huu, kwa kuwa nipo nawe. Pia Binti nitakuonesha jinsi watu wanavyofika
huku.”
Tulikwenda kwenye lango, ambapo tuliona umati wa watu
wakiangukia ndani ya shimo kubwa. Siyo elfu moja wala elfu mbili, bali wingi
wake kama mchanga wa bahari, hawana idadi! Walikuwa wananguka kwa kila sekunde,
mfano wa mkono uliojaa mchanga umwakikapo chini. Zile roho zilikuwa zinaanguka
kwa kasi. YESU alikuwa akilia, na kusema, “Binti hivi ndivyo wanadamu
wanavyopotea; hivi ndiyo mwanadamu apoteavyo!!!..... Binti, inaniumiza sana
mimi nionavyo wanadamu wanavyoangamia.” YESU akasema, “maapepo pia hufanya
mikutano huku.” Na nikasema, “mapepo yanafanya mikutano?” Yesu akasema,
"Ndiyo, Binti, wanakutana kupanga, kupanga watavyowafanya wanadamu.
Wanakutana kila siku kwa siri.” Na kwa hilo, Yesu akanipeleka kwenye sero,
15
ambapo niliona meza ya mbao na viti vikizunguka meza.
Na palikuwa na mapepo, aina zote za mapepo. Yesu akaelezea, “Binti, wanapanga
kwenda kuharibu nyumba/familia za wachungaji, wamisionari, wainjilisti na wote
wanijuao mimi. Binti wanataka kuwaharibu; wanamishale mingi.” Mapepo hucheka na
kudhihaki, na kusema, “acha tuwaharibu wanadamu na kuwaleta huku.” Yesu
akasema, “Nenda na uwaambie nipo pamoja nao watu wangu. Waambie wasiache
milango wazi, wasimpe nafasi shetani, kwa kuwa shetani anazunguka-zunguka kama
simba angurumaye, akimtafuta wa kummeza. (1 Petro 5:8)" Lakini neno
linasema, "anatembea kama", kwasababu simba halisi, ni Simba wa Yuda,
Yesu Kristo wa Nazareti (Ufunuo 5:5)! Yesu akasema, "Binti, wanataka
kuharibu/kuangamiza familia za wachungaji.” Nikamuuliza, “Kwanini wanataka
kuharibu familia za wachungaji?” na Yesu akajibu, “Kwasababu wanawajibu wa
maelfu ya watu ambao ni kondoo wa kundi; kondoo wa kundi Bwana aliowakabidhi
wao. Wanataka watu hao warudie dunia tena; waangalie nyuma na kuishia kuzimu….
Nenda kawaambie wachungaji kusema iliyo kweli tupu. Waeleze wahubiri kweli tupu
na kusema kila kitu ninachowaambia na wasinyamaze nayo haya ninayowaambia!”
Tulipokuwa tunaondoka hapo, akaniambia, “Nataka nikuoneshe kitu kingine…. Wapo
pia watoto huku.” Na nikamjibu, “watoto huku Bwana? Kwanini wawepo watoto huku?
Neno lako lasema, 'Waacheni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie: kwa maana
Ufalme wa Mbinguni ni wao." (Mathayo 19:14) Yesu akajibu, “Binti, ni
kweli, ufalme wa mbinguni ni wao, lakini mtoto lazima aje kwangu, kwa kuwa kila
ajaye kwangu sitamtupa kamwe." (Yohana 6:37) Ghafla, Bwana akanionesha
mvulana wa miaka nane akiteswa kwenye moto. Mvulana akalia, “Bwana nihurumie
mimi, nitoe mahali hapa, sitaki kuwepo hapa!” aliendelea kupiga kulia na
kelele. Nikaona mapepo yamemzunguka mtoto huyu, yaliyofanana na cartoon.
Kulikuwa na aina za Dragon, BoyZ, Ben 10, Pokémon, Doral, na nyingine nyingi.
“Bwana, kwanini mtoto huyu yuko huku?" Yesu akanionesha picha ya mkanda wa
maisha mtoto huyu. Nilimwona anavyotumia muda karibia wote kwenye LUNINGA [TV]
akiangalia cartoon. Cartoon ya Ben 10: Pokemon:
Yesu akasema, "Binti, hayo maigizo ya cartoon,
sinema zake, michezo mbalimbali ya kuigiza inayooneshwa kila siku kwenye
LUNINGA [TV] ni vyombo vya shetani atumiavyo kuwaharibu wanadamu….. tazama,
binti ilivyotokea kwa mtoto huyu." Nilimwona jinsi mtoto huyu alivyokuwa
mkaidi na asiye mtii kwa wazazi wake. Wazazi wake aliposema naye alikimbia na
kutupatupa vitu ovyo na kuto-watii. Baada ya hapo akagongwa na gari na ukawa
mwisho wa maisha yake. Yesu akasema, “Tangu hapo yupo mahali hapa.”
Nilimtazama mtoto Yule akiteswa. Yesu akasema,
"Binti, nenda na uwaambie wazazi wawaelekeze watoto wao kama ilivyo katika
neno langu.”(Mithali 22:6) Neno la Mungu ni halisi,
16
linatuambia tumwonye mtoto kwa fimbo, lakini si kila
wakati, pale tu mtoto anapoonyesha ukaidi kwa wazazi. (Mithali 22:15)
Bwana akaniambia kitu cha kuhuzunisha sana na kuumiza
mno. Akasema, “Binti, wapo watoto wengi sana huku kwasababu ya cartoon,
kwasababu ya ukaidi.” Nikamuuliza, “Bwana, kwanini lawama ziwe hizi cartoon?”
Naye akanieleza, “Kwasababu ni mapepo yanayobeba ukaidi, kiburi, ukali na chuki
kwa watoto, ili wasifanye vitu vizuri; na mapepo mengine huwaingia watoto ili
wasifanye mambo mazuri, bali wafanye mabaya: vile waonavyo kwenye LUNINGA [TV]
watoto hutaka kufanya vivyo hivyo.” Kuzimu ipo, kuzimu ni halisi, na watoto
lazima waamue watakwenda na nani. Nikasema, “Bwana, niambia, kwanini kuna
watoto huku?” na Yesu akanijibu, “Mara watoto wapatapo kujua kuna mbinguni na
kuzimu, hapo wanayonafasi ya kuchagua.”
UFALME WA MBINGUNI Kuna mengi ya kusema juu ya kuzimu,
lakini kwasasa niwashirikishe niliyoyaona Mbinguni. Yesu akasema, "Binti,
sasa nitakuonesha nilichowaandalia watakatifu wangu.” Tuliondoka kule kuzimu
kupitia lango lake. Tulipokuwa tukisafiri kutoka nje ya kuzimu, ghafla
tukatokea mahali penye mwanga. Sikuona giza tena, mateso wala miale ya moto.
Akasema, “Binti, nitakuonesha utukufu wangu,” na tukaanza kupanda juu kwenda
Ufalme wa Mbinguni! Mara tukafika kwenye mlango wenye maandishi makubwa
yaliyoandikwa kwa dhahabu, yalisema: “Karibu kwenye Ufalme wa Mbinguni.” LANGO
LA MBINGUNI
Yesu akasema, “Binti, ingia, kwa kuwa mimi ni Mlango na
kila aingiaye kupitia kwangu, ataingia na kupata marisho.”(Yohana 10:9)
Baada ya Bwana kusema maneno hayo, mlango ukafunguka na
tukaingia. Niliwaona malaika wakimpa utukufu, heshima na sifa Baba Yetu wa
Mbinguni! (Ufunuo 7:11-12) Kadri tulivyozidi kutembea, tulikaribia meza
niliyoweza kuona mwanzo wake laini siyo mwisho. (Ufunuo 19:9) Niliona enzi
kubwa, na enzi ndogo zimezungukwa na maelfu ya viti. Katikati ya viti niliona mavazi
na mataji. Bwana akaniambia, “Binti, taji unayoiona pale ni taji ya
Uzima."(Ufunuo2:10)
Yesu akasema, “Tazama, Binti, hii ndiyo niliyowaandalia
watu wangu.” Niliona ile meza imefunikwa na vitambaa vyenye upindo wa dhahabu.
Kulikuwa na sahani, glasi za dhahabu, matunda; kila kitu kimeandaliwa. Ilikuwa
nzuri ajabu. Kulikuwa na chombo kikubwa katikati ya meza, kilichokuwa na mvinyo
tayari kwa mulo. Na Yesu akasema, “Binti, kila kitu kipo tayari kwa ujio wa
kanisa langu.”
17
MEZA YA KARAMU YA MBINGUNI
Tulikwenda mahali pengine, niliwaona watu wengi wakiwa
bustanini. Kulikuwa na watu wanaofahamika sana kwenye Biblia, lakini hawakuwa
wazee, bali vijana. Palikuwa na kijana akiwa na kitambaa mkononi, akicheza na
kuzungukazunguka na kumsifu Bwana. Yesu akasema, “Binti, Yule kijana pale ni
mtumishi wangu Daudi.” Alikuwa akimpa utukufu Baba yetu. Ghafla, kijana
mwingine akapita na Yesu akaniambia, “Binti, huyu ni Joshua; Yule Musa; na Yule
pale ni Ibrahimu.” Yesu huwaita kwa majina yao. Wote walikuwa na mwonekano
mmoja! Ajabu sana Mbinguni! Yesu akasema, “Mwanamke Yule ni mtumishi wangu,
Maria Magdalena; na Yule mtumishi wangu Sara."
Lakini pia akaniambia, “Binti, huyu ni Maria. Maria,
aliyemzaa Yesu Kristo, ambaye ni mimi. Binti, nikwambie, yeye hana habari ya
yanayotokea duniani. Nataka kukwambia, nenda kawaambie wanadamu, waambie
waabudu sanamu kuwa kuzimu ni halisi, na waabuduo sanamu hawata urithi Ufalme
wangu, lakini waambie kama wakitubu, wataweza kuingia makao ya mbinguni. Nenda
waambie nawapenda na pia waambie Maria hajui chochote [kinachotendeka duniani]
na pekee wanayeweza kuheshimu ni mimi, kwasababu si maria wala mtakatifu
Gregory wala mtakatifu yeyote awezaye kuokoa. Mimi ndiye niokoaye na nje yangu-
hakuna yeyote, hakuna yeyote, hakuna yeyote – aokoaye!” Alirudia mara tatu-kuwa
hakuna yeyote awezaye kuokoa; isipokuwa yeye. Wanadamu wamedanganywa na kuamini
kuwa kwa kupitia wadhaniwao ni watakatifu, sivyo ilivyo, bali ni mapepo,
yafanyayo kazi kupitia sanamu zilizofanywa kwa mikono ya watu. Lakini ngoja
nikueleze kwamba Bwana anataka kukupa kilicho bora. Anataka wewe uingie katika
Ufalme wa Mbinguni; tubu na kuacha uabudu sanamu. Kwasababu ibada ya sanamu
haitakuokoa wewe. Yesu Kristo wa Nazareti ndiye pekee aokoaye, aliyeutoa uhai
wake kwaajili yako, yangu na kwaajili ya wanadamu wote. Bwana ana ujumbe mzito
kwa wanadamu. Huku akilia aliniambia, “Tafadhari, Binti, usikae kimya; nenda na
uwaambie ukweli, nenda na uwaambie nilichokuonesha wewe.” Sanamu za Maria na
Waumini wa kisujudia
Nilimwona Maria akimwabudu Bwana, na niliwaona wanawake
wakiwa na nywele ndefu nzuri. Nikasema, “Bwana, wanapendeza sana walivyoweka
nywele zao.” Akaniambia, “Binti, kile uonacho ni utaji niliowapa wanawake.”
Akaongeza, “Binti, nenda na uwaambie wanawake watunze utaji niliowapa.”
18
Kisha akaniambia, “Nina kitu cha muhimu cha
kukuonesha.” Nikatazama mbali kidogo na kuona MJI UNG’AAO, MJI WA DHAHABU!
Nikasema, “Bwana, kile ni nini? Nataka kwenda pale.” Akanijibu, “Binti,
nitakuonesha kilichopo pale. Ukionacho ni makao ya Mbinguni, majumba ya
Mbinguni yaliyotayari kwaajili ya watu wangu.” Tulianza kutembea, hadi tukafika
kwenye daraja la dhahabu. Mara tulipovuka daraja, tukafika kwenye mitaa
iliyotengenezwa kwa dhahabu safi! (Ufunuo 21:21)
Kila kitu kilikuwa kizuri sana, kuzuri sana pale,
kunang’aa kama kioo, ni mahali pasipo pakawaida, hakuelezeki! Tuliona majumba
ya ki-mbinguni na pia tuliwaona, maelfu ya malaika wakijenga. Baadhi ya malaika
walikuwa wanajenga kwa haraka ya ajabu, na wengine pole pole na wengine walikuwa
wamesimama kabisa kujenga. Nikamuuliza Bwana, “Kwanini malaika wengine
wanajenga haraka haraka, wengine polepole, na wengine wamesimama?" Bwana
akanieleza, “Binti, hivyo ndivyo wafanyavyo watu wangu duniani, na malaika
wanafanya kama wafanyavyo watoto wangu duniani…. Binti, watu wangu hawahubiri
neno langu. Watu wangu hawafungi tena. Watu wangu hawaendi mtaani kusambaza
ujumbe wa neno langu kwa vipeperushi vinavyoeleza ukweli. Watu wanaona aibu
kuhubiri. Nenda kawaambie watu wangu warudi kwenye njia za zamani. Wale malaika
uliowaona hawafanyi chochote ni malaika wa watu wangu waliorudi nyuma na kuacha
njia zangu… Binti, nenda waambie watu wangu warudi njia zao za zamani,”
(Yeremia 6:16) na baada ya kusema haya akaanza kulia Bwana.
Nikasikia watu wengine wakiimba, hivyo nikamuuliza,
“Bwana, nataka unipeleke kule, ambako watu wanaimba.” Yesu alikuwa
akiniangalia, nakwambia jinsi alivyokuwa ananiangalia, sikuweza kuona vema uso
wake bali alikuwa akigeuza uso wake. Wakati huo machozi yalikuwa yakimtiririkia
kwenye vazi lake, nikamuuliza kwanini analia. Lakini hakuweza kunieleza.
Baadaye tulifika kwenye bustani nzuri sana. Pale katika
majumba ya mbinguni, niliona maua yalikuwa yakiyumbayumba huku na huku kama
yapulizwayo na upepo. Hizi huenda ndizo sauti za kuimba nilizozisikia. Bwana
akaninyoshea kidole na kusema, “Binti, tazama, maua yananisifu mimi;
yananiabudu mimi! Watu wangu hawafanyi hivi tena kama walivyokuwa wanafanya
mwanzo. Watu wangu hawanisifu, hawaniiabudu mimi; hawanitafuti mimi kama
mwanzo. Ndiyo maana nalikwambia mwanzo, Binti, nenda na uwaambie watu wangu
wanitafute, kwa kuwa nitakwenda, nitakwenda, nitakwenda kwa wanaonitafuta kwa
roho na kwa kweli, kwa watu walio tayari, kwa watakatifu!” na huku akilia
akasema, “Ninakuja, ninakuja!” hapo nikaelewa kwanini alikuwa analia, kwasababu
anakuja, lakini si kwa wasio na nia, watu wa nia mbili [vuguvugu]. Atarudi kwa
wale tu wanaomtafuta katika roho na kweli.
Ndipo Bwana akaniambia ninatakiwa kurudi duniani.
Nikasema, “Bwana, Sitaki kurudi duniani! Unamaanisha nini- duniani? Nataka
kubaki na wewe Bwana. Umenileta huku na mimi siendi kokote kwasababu niko na
wewe!” Yesu akasema, “Binti, ni muhimu urudi duniani ili ukashuhudie kwamba
utukufu wangu ni halisi, yote niliyokuonesha kuwa ni kweli; ili wanadamu waje
kwangu, watubu na wasiangamie.” Bwana akaanza kulia, nami nikaanguka miguuni
pake; nikaona vidonda kwenye miguu yake. Nikamuuliza, “Bwana, hivi ni vidonda
vya nini?” akajibu, “Binti, ni vidonda ya jana, nilipotoa maisha yangu kwaajili
ya wanadamu.”
19
MKONO WA YESU
Bwana akanionesha vidonda vyake vya mikononi,
nilimuuliza, “Bwana, kwanini ungalinavyo hata sasa?” akaniambia, “Binti, ni
vidonda vilivyobaki.” Hivyo nikamuuliza, “je vitapona?” akanijibu, “Vitapona na
kufutika tu baada ya watakatifu wote kuungana hapa….. Binti, lazima nikurudishe
duniani: Familia yako na mataifa yanakusubiri wewe.”
Nilijaribu kukataa lakini akanyosha kidole chake chini
duniani na kusema, “Tazama, wale watu uwaonao chini pale ni ndugu zako; na
mwili ule uuonao pale, ndiyo utakaoingia…… ni muda wa kuondoka mahali hapa.”
Baada ya hapo akaanipeleka kwenye mto mzuri mwangavu na akasema, “Binti, ingia
katika mto na jizamishe mwenyewe.” Kabla sijaingia ndani ya mto wa maji ya
uzima, nilikuwa najisikia furaha ya ajabu, lakini baada ya kujizamisha na
kutoka nje, nilipata furaha kuu. Nilidhani sitarudi tena nyumbani kwetu, lakini
Bwana akaniambia, “Binti, unatakiwa kurejea duniani….. Binti, nitakuonesha
kitu: jinsi nitakavyorudi mara ya pili kwaajili ya watu wangu watakatifu. Nitakuonesha
jinsi siku ile ya kutisha itakavyokuwa.”
FURAHA NA MAOMBOLEZO Tulitembea hadi sehemu yenye kioo
kikubwa kama LUNINGA [TV], nikaona watu. Niliweza kuona dunia yote. Ghafla
nikaona maelfu ya watu wakipotea. Wanawake wenye mimba, mimba zilipotea, na wakawa
kama wamechanganyikiwa na kupiga mayowe.
Watoto walitoweka pande zote. Watu wengi walikuwa
akikimbia huko na huku, wakipiga kelele, “Haiwezekani, haiwezekani, nini hiki
kitokeacho?”
Niliwaona wale waliomjua Bwana na kuachwa nyuma.
(Mat.24:40-41) Walikuwa wakisema Kristo amekuja, furaha imetimia. Walikuwa
wakipiga kelele na kutafuta kujiua wenyewe lakini hakuwezekana. Bwana
akaniambia, “Binti, siku hizo kifo kitawakimbia; Binti, siku hizo Roho
Mtakatifu hatakuwepo tena.” (Ufunuo 9:6) kulikuwa na ajali nyingi lakini
sikuona hata mtu mmoja aliyekufa: wote walikuwa wazima japokuwa wameumia
[majeruhi].
Niliona mlolongo mrefu wa maelfu ya watu. Akaniambia,
“Binti, tazama, hivi ndivyo kila kitu kitakavyokuwa.” Kisha nikaona watu
wakikimbia kutoka sehemu moja kwenda nyingine, wakipiga kelele, Kristo kaja,
Kristo kaja!” wakisihi, “Bwana nisamehe mimi, nisamehe mimi, nichukue nawe!”
20
Baada ya Bwana kuwachukua watu wake [Unyakuo]
Lakini kwa huzuni Bwana akasema, “Watakuwa wamechelewa.
Muda wa kutubu ni sasa…. Binti, nenda kawaambia wanadamu wanitafute mimi,
wakati huo hakutakuwa na nafasi. (Isaya 55:6) Binti, watakuwa wamechelewa wote
watakaobakia nyuma.” Baada ya Yesu kuona watu wataobaki nyuma akaanza kulia na
kusema, “Binti, nitakwenda duniani kama neno lisemavyo katika 1 Thes. 4: 16-17:
“Kwasababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti
ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo
watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao
katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana
milele. Basi farijianeni kwa maneno hayo.”
SIKU YA MWISHO
Lakini si kila mtu atakwenda na Bwana, wale tu wafanyao
mapenzi yake (Mathayo 7:21) na aishiye maisha matakatifu. Kwa kuwa Bwana
aliniambia, “Wale tu walio watakatifu wataoingia Ufalme wa Mbinguni, (Waebrania
12:14) Hakuna ajuaye, siku wala saa nitakayokuja kwaajili ya watu wangu
watakatifu, hata malaika hawajui.” (Mathayo 24:36)
Kwenye Kioo cha LUNINGA [TV] niliona watu wakikimbia
huko na huku. Magazeti yalisema “KRISTO AMEKUJA.” Kioo kikafungwa, na Yesu
akamalizia kwa kusema, “Ninakuja kwa watakatifu.” Hivi ndivyo alivyonionesha
mimi. Baada ya hapo akanirudisha duniani hapa. Tukiwa na kusanyiko la malaika
wengi wakituzunguka, tulianza kushuka ngazi nzuri kama nini; ngazi nyeupe na
maua yakizunguka. Nilikuwa nalia njia nzima kushuka chini, nikimsihi Yesu,
“Bwana tafadhari usiniache hapa. Nichukue niwe nawe!” Alinijibu, “Binti,
mataifa yanakusubiri, familia yako wanakusubiri wewe…….. Binti, lazima urejee
mwili wako. Lazima upokee uhai wako, Binti, ili uweze kwenda kushuhudia yote
uliyoyaona. Wengi hawatakuamini wewe; wengi watakuamini, bali mimi ni shahidi
wako mwaminifu. Niko pamoja nawe. Sitakuacha kamwe."
21
KURUDI DUNIANI KWA ANGELICA Maxima: Binti yangu
aliporudi, tulikuwa tunamsubiri pale, na alikuwa amelazwa pale pale chini
sakafuni. Nikasikia mguno, "uuhmm," bila kitu. Nikasema, “ahsante
Bwana kwasababu Binti yangu amerudi!”
Sote tulimshukuru Bwana. Mara akaanza kupumua polepole,
kidogo kidogo. Baada ya muda wa masaa matano, alikuwa na uwezo wa kufumbua
macho na kusema. Mwanzo tulipata shida kumuelewa asemacho; ilikuwa ni vigumu
kumuelewa. Hakuwa na nguvu kabisa. Ilibidi tufunge madirisha kwasababu macho
yake hayakuwa na uwezo wa kuhimili mwanga.
Kwakuwa wadadisi, sote tulitaka atueleze alichoona.
Lakini kwa kuwa alikuwa dhaifu, aliweza kutueleza kidogo tu. Ilimchukua karibu
wiki mbili hadi alipoweza kutushirikisha habari nzima ya ushuhuda wake.
Mapepo yalikuja kumtesa baada ya hayo yote. Aliweza
kuyaona waziwazi; yalijaribu kujificha kwenye vivuli. Yalikuwepo hapa karibu
siku tatu mfululizo tangu arudi, kabla hajaweza kutueleza. Aliyauliza yalikuwa
yanataka nini, nayo yakamjibu, “tumekuja kufanya mkataba nawe……. Ni lazima
ufunge mdomo, ni lazima usiseme lolote ya hayo uliyaona kule chini, kwasababu
ukisema, tutakuuwa.” Aliyaelezea yalivyo mapepo, yana sura mbaya, makubwa na
manene yanatisha. Alisema hakuna maneno yakuelezea jinsi yatishavyo kwa
mwonekano. Alijaribu kuyakemea lakini yalikataa kuondoka. Yakifika yalikuwa
yanamrukia na kumchoma. Naye aliendelea kupambana nayo na kuyakemea, lakini
hakuweza kwasababu hakuwa na nguvu. Siku moja alipokuwa anayakemea, mwanga
mkali wa ajabu ulitokea na yakakimbia yote! Alikuwa ni Bwana.
Alichopitia Binti yangu hakikuwa rahisi. Alipewa ujumbe
wenye maono ya ndani kwaajili ya wanadamu, ili wamtafute Mungu. Wanadamu
wanadhani wafanyayo ni sahihi. Vijana wamezama kwenye madawa ya kulevya na
pombe, na kuona ni sawa maisha hayo, lakini si sawa. Miongoni mwa alioneshwa
binti yangu ya kutisha ni wasanii wengi walivyojaa kuzimu, wanamuziki/wacheza
dansi na pia Papa John Paul II. Ni wakati wa kumtafuta Bwana, kutubu, na
kujishusha na kujidhiri mbele za zake. Neno la Mungu ni kweli lisemalo, “Mbingu
na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”(Mark 13:31) Neno la
Bwana litatimizwa katika muda wake. Bwana alimwonesha tanuru ambalo watu
walikuwa wanatembea kuelekea kuzimu. Na watu wengi tayari wakiwakuzimu. Ni
kweli haya, lakini hata watu wa Mungu hawaamini haya, wengi hawaamini.
Ujumbe mkuu ni kwamba tumtafute Bwana, siyo kwa
kinywa/mdomoni, bali kutoka ndani ya moyo, kwakuwa kurudi kwa Bwana ku-karibu.
Yesu alisema, “Siko tena mlangoni; niko zaidi ya mlangoni. Nakuja muda simrefu;
kuja kwangu ku-karibu. Watu wangu wameniacha na wamerejea mambo ya duaniani………
waambie watu wangu warudie njia zao za zamani.”
22
Kanisa leo linatakiwa kurudia njia zake za zamani; hapa
tulipo ni wa motoni, tumtafute Bwana. Pale parapanda ikilia tuwe tayari
kukutana na Bwana, itakuwa ajabu sana!
UJUMBE WA MUHIMU WA BWANA
Angelica akiongea mbele ya haraiki: Bwana akaniambia,
“Binti, siku hizo Roho Mtakatifu hatakuwepo tena duaniani. Siku hizo hatakuwepo
duniani.” (2 Thes. 2:7) Na nikaona msongamano mkubwa wa magari na ajali nyingi
sana. Watu wengi walijaribu kujiua, lakini Yesu akasema, “Watatafuta kifo,
lakini kifo kitawakimbia wanadamu. Kifo hakitakuwepo tena siku hizo.”(Ufunuo
9:6) Nikawaona watu wakitazama LUNINGA [TV] na kusoma magazeti yakisema,
“Maelfu na maelfu wamepotea.” Wengi watajua kuwa Yesu ameshakuja kwaajili ya
watu wake watakatifu. Wale waliomjua Bwana lakini wameachwa, wakakimbia mitaani
wakilia, wakijaribu kujiua wenyewe lakini hawakuweza lolote.
Nilipokuwa mbinguni, Yesu alisema, “Nina kuja duniani
kwaajili ya watu wangu watakatifu na ninakuja mapema kwaajili ya kanisa langu.”
Lakini wiki mbili zilizo pita Bwana aliniambia, “Binti, ninafurahishwa na
unavyotenda, kwa kuwa unatimiza niliyokuagiza na nakukupa, lakini usiwaambie
watu wangu kuwa nitakuja mapema, waambie ninakuja sasa hivi.” Tena Bwana
akasema, “Waambie watu wangu ninakuja sasa hivi na ninakuja kwa watu watakatifu.
Waambie watu wangu nakuja kwa watakatifu tu, nao ndio wataoniona mimi!.... tena
usinyamaze: endelea kuwashuhudia ninayokwambia.”
Angelica akiomba na haraiki: Kila mmoja afumbe macho,
na weka mkono wako wa kuume kifuani. Inua mkono wa kushoto juu, kama unajisikia
kulia[toba], lia tu. Sasa mweleze Bwana kile unachojisikia moyoni. Kwa wale
waliotayari kumpokea Bwana, wafuatiane nami ktika maneno haya: Bwana,
ninakushukuru kwa Upendo na huruma yako, ahsante Bwana kwa maneno yako
yaliyotufikia mioyoni leo. Baba, ninaomba msamaha kwako, unisamehe. Unisamehe
mimi. Unioshe kwa damu yako ya thamani. Andika jina langu katika kitabu cha
uzima. Nipokee/nikubali mimi niwe mwanao Bwana. Sasa hivi, ninamsamehe kila mtu
niliyeshindwa kumsamehe. Ninakana hali yangu ya kutosamehe. Ninayakana yote
yalinizuia nisikufuate Bwana, ninaomba unibadilishe Bwana na unijaze uwepo wako
ndani yangu kila siku. Ahsante Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Ameni.
23
Angelica: Ushuhuda huu siyo uwongo; siyo mzaha; siyo
hadithi; siyo ndoto, kuzimu ni kweli ipo! Kuzimu ni halisia! Kwa yeyote
asiyeamini, nataka kukueleza kuzimu ni kweli ipo, ni kweli ni halisi. Ninakosa
maneno zaidi mazuri ya kuelezea uhalisia wa kuzimu. Natamani kama ungeshuhudia
wewe mwenyewe. Lakini tafadhari amini, tii na uonyeke kwa ushuhuda huu
[ushuhuda ukuonye na kukubadilisha] ili uepuke moto wa milele.
Angelica akiongea na Mfasiri/Muelezeaji: Muda ukaribu
sana, Mungu anaruhusu ishara kwa wanadamu zitokee ili kuwaonesha
kitakachotokea. Usibakie ukihukumiwa; ndilo shetani atakalo. Jiulize kama uko
tayari ukitembea kuelekea shimo la kuzimu? Leo ni siku ya wokovu, leo ni siku
ya kumkaribisha Yesu, kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako. Haya ni maneno
rahisi lakini ni makubwa sana kusema: “Ninakubali na kukupokea Yesu uwe Bwana
na Mwokozi wangu. Ninakupa wewe maisha yangu na roho yangu kwa moyo wangu wote.
Natakuwa kuwa nawe kwa maisha ya milele.”
Chagua hatima yako baada ya maisha haya: Uzima au
mauti, Mbinguni au kuzimu, Yesu au shetani. Iko wazi, uko upande wa Yesu au
upande wa shetani. Au unafanya yaliyo mema au unafanya yaliyo mabaya. Chagua
mwisho wako: uzima wa milele au ziwa la moto. Fikiria jambo hili. Fanya uamuzi
sasa. Yesu Kristo alikufa msalabani kwaajili yetu, kwa dhambi zetu, na akatupa
fursa ya wokovu kwa huruma yake. Mpokee Yesu Kristo kuwa mwokozi wako!
“Sasa umesikia ushuhuda huu, usiipoteze nafasi hii
ukaijutia milele na milele motoni.”
Marejeo:
Ufunuo 19:9 ….Heri walioalikwa karamu ya arusi ya
mwanakondoo. ……..maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.
Ufunuo 20:15 Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa
katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. Ufunuo 21:4 Naye
atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwepo tena; wala
maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwepo tena; kwa kuwa mambo ya
kwanza yamekwisha kupita.
Ufunuo 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa
maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari
tena.
Ufunuo 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao,
na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote,
sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya
pili.
“Hakuna waabuduo sanamu wataourithi ufalme wa
Mbinguni.”
Kutoka 20:4-5 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala
mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala
kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi,
Bwana, Mungu wako, ni Mungu wenye wivu……..
Ufunuo 21:21 Na milango kumi na miwili ni lulu kumi na
mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo
kiangavu.
Ufunuo 21:27 Na ndani hakitaingia kamwe chochote
kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika
kitabu cha uzima cha mwana koondoo wa Mungu.
Ufunuo 22:7 Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye
maneno ya unabii wa kitabu hiki.
Ufunuo 22:11 Mwenye kudhuluma na azidi kudhulumu; na
mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na
mtakatifu na azidi kutakaswa.
Ufunuo 22:12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u
pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
Ufunuo 22:13-15 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na
mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri ya
kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako
mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu
apendaye uongo na kuufanya.
Subscribe to:
Posts (Atom)