NILINUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUBADILI DINI
 |
ESTER |
Naitwa Ester Mahamud japokuwa zamani kabla sijaokoka niliitwa Aisha
mahamud nina miaka 21 nimzaliwa wa moshi mkoa wa kilimanjaro,Ninaishi
Dar es salaam napenda kuwashuhudia jinsi nilivyotaka kuuawa na mama
yangu mzazi kwa kushirikiana na ndugu pamoja na majirani. Mama na baba
walitengana nikiwa mtoto mdogo na mimi na mama tukaenda kuishi Zanzibar
na baada ya kufika huko mama aliolewa na mwanaume mwingine na maisha
yaliendelea kama kawaida.Nikiwa na miaka 15 nilianza kuumwa kichwa na
kupagawana na mapepo hali hii iliendelea kwa muda mrefu na mama
alinipeleka kwa waganga wengi wa kienyeji lakini sikupona .Hali hiyo
ilinisumbua sana kwani wakati mwingine nimevaa vizuri lakini nikipagawa
tu nakujakujikuta nimechafuka sana pia nilikua nasumbuliwa na ndoto za
kutisha mara kwa mara. Mwaka 2008 tulipanga safari ya kwenda kilimanjaro
na tulilala Dar es salaam kwa kaka na siku hiyo nimelala chumba cha
jirani kulikua radio inaongea na ilikuwa WAPO FM na wakati mhubiri wa
kwenye radio anamalizia kufundisha alisema yeyote aliyeko majumbani
anayeumwa chochote au kusumbuliwa na chochote aweke mkono kifuani na
yeye ataomba niliweka mikono yangu kifuani na wakati mchungaji huyo
anaomba nilihisi kuna vitu vinatoka mwilini mwangu na baada ya maombezi
hayo kwa njia ya radio nilijihisi kuwa mzima japokuwa mimi sikuwa
mkristo ila nilitaka tu kupona. Baada ya hapo nililala na kuamka salama
na kesho yake tulienda moshi na baada ya wiki3 tulirudi na kulala
hapohapo kwa kaka kwani tusingeweza kupitiliza zanzibar moja kwa moja.
Pia kumbuka nikiwa kilimanjaro siku moja majini walikuja na kunionya juu
ya kujihusisha na ukristo kwani nikiendelea wataniua na kesho yake
nikiwa hukohuko moshi nilijisikia wa tofauti kama nataka kufamiwa na
majini na hiyo nilijua kwa sababu ya kuvamiwa na majini kwa muda mrefu
sana hadi nikajua ishara zao kama wakitaka kunivamia na baada ya kuhisi
hivyo nilianza kuomba kwa dini yangu sala zote lakini hali ndio ilizidi
na wao majini walianza kunicheka lakini hata sijui nilikumbukaje yale
maneno ya yule mhubiri radioni nikajikuta natamka ''kwa jina la YESU''
wale majini walipiga kelele na kusema wanaungua na kuniambia nisitaje
hilo jina tena kwani ndo jina pekee ambalo ni kikwazo kwao. Baada ya
kufika kwa kaka tukiwa safarini kurudi nyumbani Zanzibar usiku ule
kulikua na hali sio ya kawaida kwani niliweza kuwaona majini na wachawi
live na nikaogopa sana ila nikajua kwamba yule YESU wa wakristo ndie
kiboko ya wachawi na majini wote lakini siku hiyo hata sijui walinifanya
nini kwani hata kutamka nilishindwa na kile chumba ambacho siku ile ya
kwanza walifungulia RADIO WAPO siku hiyo haikuwa hivyo na nililala na
watoto wa kaka ambao hawakujua chochote kilichokuwa kinaendelea ila
walikua tu wanakoroma kiukweli siku hiyo sikulala kabisa ila usiku wa
manane kwenye chumba kile jirani nilisikia mtu anaomba na kukemea nguvu
zote za giza zilizopo maeneo hayo walikua na mke na mme na waliendelea
kuomba na mimi kwa sababu nikuwa na uwezo wa kuwaona majini na wachawi
nishuhudia moto ukishuka kutoka mbinguni na kuwateketeza wale majini.
Baada ya muda pakawa shwari na muda huo huo baada ya hari kuwa shwari
mama alipiga simu na kuanza kuongea kwa hasira kwamba kwanini nashiriki
kuwaharibu wenzake? nilimuuliza kivipi alisema kwa sababu namtaja YESU
wakati mimi sio mkristo kiukweli sikumwelewa mama na nikawaza sana kwani
hata nikiwa huko aliko yeye yaani zanzibar hakuwa ananijali na
akaniambia nijiepushe kuwa karibu na wakristo. Kulipokucha asubuhi
niligundua kuwa yule aliyekuwa anaomba chumba cha pili ni mchungaji
kijana ambaye amepanga kwenye nyumba hiyo na nilitamani kumshukuru kwa
maombi yake yaliyonisaidia sana hata kama yeye hakujua kama ameniombea
na mimi Na kiukweli muda wote nilikuwa nawaza mama kajuaje na kwanini
hao majini ni wenzako. Kesho yake nilipanda bot na kurudi zanzibar, mama
alinifokea sana na nilikaa kwenye ulinzi mkali sana na pia alitumia
muda mwingi sana kuwasema vibaya wakristo pamoja na ukristo yeye pamoja
na mmewe ambaye ni kiongozi wa dini. nilikaa kwa miezi kadhaa na hali
yangu ya kupagawa na kumwa kichwa ilirudi na mama aliniambia kuwa hawezi
kunipeleka tena kwa waganga kwani mganga wa mwisho alimwambia
wameniwekea majini mengi mno hivyo kwenda kuongeza jini jingine hataki.
kwa kusikia hivyo niliogopa sana na kulia sana huku naumwa. Baada ya
muda walikuja vijana 2 wakristo wakishuhudia na mama aliwatukana sana
lakini wakasema ubarikiwe mama nilitamani sana kuwafuata lakini
nilishindwa. Baada ya muda nilipanga kutafuta kazi za ndani ili nipate
nafasi ya kuombewa ili nipone kwani kama kwa maombezi ya radio nilipona
kwa muda pia maombezi ya yule mchungaji kule Dar nilipona kwa muda mrefu
na hadi mama akalalamika hivyo niliuaga mama na kwenda kutafuta kazi ya
ndani na nikapata kazi hiyo kwa nyumba ya mkristo japokuwa walikuwa ni
wakristo jina tu kwani sikuwaona kujihusisha na kanisani.Nikiwa pale
niliwaona wale vijana wahubiri na kuwaomba namba zao za simu na baada ya
hapo nilienda kanisani na niliombewa na kupona kabisa hakika hakuna
kama YESU KRISTO na hatatokea kama yeye milele na tangu muda huo
niliokoka hadi sasa naendelea na wokovu bila kuonewa na nguvu za giza
hata siku moja hakika ukiokoka unakaa salama kabisa nje ya uonevu wowote
wa wachawi. Baada ya kuokoka mama alifahamu na kuanza kunikusanyia watu
ili waniue na alikuja hata nilipokuwa nakaaa na kumweleza mwenye nyumba
na mwenye nyumba akanifukuza huku mama akinitafuta zaidi ya mara 4
kuniua lakini MUNGU BABA tu ndie aliniepusha na kifo. Pia mama
aliniambia kuwa undugu kati ya mimi na yeye umekufa na yeye sio mama
yangu tena hivyo nitafute mwingine. Niliishi kwa mmoja ya waumini wa
kanisa lakini nikitafutwa kuuawa kwa sababu nimekubali kujiunga na
ukristo. nilikaa zanzibar lakini nilipozidi sana kutafutwa ili niuawe
maana nilikua nashinda ndani. Ndipo kanisa likanipa nauli na nikaja
kuishi Dar es salaam ambako naishi hadi sasa huku nikiwa nimeokoka na
namshukuru MUNGU BABA kwani kanibariki na kunipa mchumba na mwezi
uliopita mama alikuja kuniomba msamaha na kuniambia kweli amehakikisha
kuwa kuokoka ndio dini ya kweli kuliko zote tena akaniambia kuwa yeye ni
mchawi na amejaribu zaidi ya mara 10 kuniua lakini aliwakuta malaika
wakinilinda na ametumia wakuu wake wa uchawi zaidi ya watano lakini
wameshindwa hivyo anaomba tu nimsamehe lakini yeye hawezi kuokoka kwa
sasa labda baadae. SIKU ZOTE NINAOMBA NA NAAMINI IPO SIKU MUNGU
ATAMWOKOA.MUNGU awabariki sana na kama hujaokoka ndugu tangu leo tambua
kuwa hakuna jambo zuri kama kuokoka na mbinguni ni hakika pia jehanamu
na hakika lakini kama tukimpa BWANA YESU maisha yetu hakika tuna uzima
wa milele. Amen.
CHANZO: www.maishaushindi.blogspot.com
No comments:
Post a Comment