MSALABA
Lengo kuu: Kujua
Maana, Sababu na Nguvu ya Msalaba.
Lengo Mahsusi:
Kila Mkristo kujua uwezo ulio ndani ya msalaba.
Swali: Msalaba
unaweza kukukinga na mashambulizi ya shetani?
Nini
maana ya Msalaba?

Dhana ya Msalaba,inafasiliwa kwa utofauti kulingana na mtazamo wa jamii hiyo na pengine
mapokeo yao. Hivyo, maana ya msalaba,hutegemea na wakati na mazingira. Kwa
dhana hii, hatuwezi kupata maana moja ilinayounganisha jamii zote na nyakati
zote.
Zifuatazo ni baadhi ya fasili
za Msalaba:
Uamuzi mgumu :- maana hii ilitolewa na Yesu mwenyewe katika (Luka 14 :17) ikimaanisha gharama
kubwa sana, ambayo ni sharti mtu atulie
na kuitafakari kwa kina. Hii inatupa kujifunza kuwa, kuuchukua msalaba si suala
la mchezo, ni suala linalohitaji maandalizi. Pengine niweke wazi kuwa, wokovu,
si kitu cha kukurupuka, wala kuigiza, bali yakupasa kujitafakari kwa kina na
kuchukua uamuzi moyoni mwako kwa kumaanisha.
Msalaba ni Laana :- Wayahudi waliamini kuwa, msalaba ni ishara ya
kukataliwa katika jamii yote. Yaani, kutokukubalika katika jamii. Na kifo cha
msalabani, ni kifo cha aibu sana mapochoni pao. Msalaba ni ishara ya kutokufaa
katika jamii yote. Kifo hiki cha msalabani, alihukumiwa mtu asiyefaa kabisa kwa
kiwango cha juu kabisa. Ni kifo kilicho dharauliwa kuliko hata mbwa. Ni kifo
cha kudharirisha alichositahiri mtu aliyekithiri kwa uovu wake katika jamii
yote. Pengine kifo hiki, kilifanyika kwaajili ya kukomesha tabia ya
aliyehukumiwa. Kama ni mwizi, basi ilifanyika hivi ili kukomesha wizi, na kama
ni mchawi, kwaajili ya kukomesha uchawi. Kwa maelezo hayo, tunang’amua kuwa,
kifo cha Yesu Msalabani,kililenga kukomesha Ukristo (tabia za Kristo) duniani.
Maana yake, ni kutokukubaliana na kile alichokuwa akitenda duniani. Na kwa
hatua hii, ni laana kwake na kwa wafuasi wake wote. Pia, hii iliachilia mlango
wazi kutendewa hivi yeyote atakayeonekana, kumfuata Yesu.
Kubeba mzigo mzito sana :- jamii nyingi, hata
fasili aliyotoa Yesu utabaini kuwa, msalaba, unahusishwa na mzigo mzito
sana,ambao hayubebeki, mzigo ambao kwa hali ya kawaida,hauwezekani,isipokuwa
unalazimika kuubeba. Ijulikane kuwa, hata Yesu, kuna kipindi alifikia hatua ya
kutokutaka kuubeba msalaba, isipokuwa kwa mapenzi ya Baba tu, ndipo aubebe(Mahayo 26 :42). Kwa mtazamo huo,
tunabaini kuwa ni dhahiri, kwa wakati ule na mazingira yale, msalaba ulikuwa na
maana hiyo kwa jamii hiyo.
Kwamaana hiyo
swali lakujiuliza ni je, kama huo ndio ukweli wake, inakuwaje, mtu anavaa
msalaba, na pengine hata kwenye kaburi unakuta umewekwa msalaba ?
Inamaana, mtu anaaamua kubeba mzigo wake mwenyewe siku zote ? au ndugu wa marehemu wanamtwika ndugu zao
mzigo ? Lazima jibu liende mbali ya hapo zaidi.
Ukweli ni
kuwa, pamoja na dhana hizo zote, kuwa msalaba ni laana, msalaba ni mzigo
mzito,msalaba ni uamzi usio wa
kawaida, kwa ulimwengu wa leo, Msalaba ni Ukombozi, Msalaba ni Ushindi,
Msalaba ni kuwekwa Huru. Kwa fasili hii, tunapata maana
moja,inayounganisha jamii zote, maeneo yote na nyakati zote na tamaduni zote.
Na hii ndiyo sababu, unakuta mtu amevaa msalaba,mwingine amepamba kwenye nyumba
yake, au kwenye gari amechora msalaba. Hata kwenye kaburi, anaweka msalaba,
japo wengine wanafanya hivyo tuu, kama ishara ya dhehebu flani, au kinga ili
wasivamiwe na mapepo, ila ukweli unabakia kuwa wazi kwamba, msalaba wa kweli,
unaanzia rohoni wala si vazi au urembo flani.
…akisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya
kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu,akaiondoa isiwepo
tena,akaigongomea msalabani (Wakolosai 2 :14). Kupitia kifo cha
Yesu msalabani, tunapata kuona kuwa, hati yetu ya mashitaka iliondolewa,
tuliwekwa huru. Mashitaka yetu,yaligomgomewa msalabani. Dhambi zetu, zilichukuliwa
pale msalabani, kifo cha Yesu msalabani,kilipelekea ulimwengu kuhesabiwa haki.

Kwanini Yesu alikufa msalabani wala si kifo
kinginecho ?
Pamoja na Yesu
kuja kwetu kwa upendo, kwa wema mwingi, akafanya miujiza mingi lakini kwa
wayahudi,bado alionekana hafai,pamoja na kuwaponya ndugu zao,pamoja na
kuwafufua ndugu zao waliokufa, lakini bado, walimwona hafai, wakamkataa. Hata
Pilato alipouliza, kati ya Yesu na Baraba, afunguliwe nani ; wakapaza
sauti zao kwa pamoja ‘ afunguliwe Baraba’ hii inamaana kuwa, walimkataa
Yesu,wakamkubali Baraba, wakamwona Baraba ni bora kuliko Yesu.
Nia ya
wayahudi,ilikuwa kummaliza kabisa Yesu na kufuta Historia yake kabisa kwenye
ulimwengu watu waliowahi kutenda jambo lolote jema. Walilenga kuanzisha
Historia mpya juu yake, endapo atakumbukwa, basi akumbukwe kwa uovu wala si kwa
wema. Kumbe mawazo ya Mungu, si ya mwanadamu, nia ya Mungu, na njia zake hakika
hazichunguziki, ukuu wake ni wa ajabu mno; na mawazo yake si sawa na mawazo ya
binadamu. Nia ya Mungu ilikuwa kumkomboa
mwanadamu, ilikuwa kumweka huru aliyefungwa. Baada ya Yesu kukamatwa, hati
mauti ya msalaba ya Baraba, ikafutwa mara moja.
Kuachiliwa kwa
Baraba kulimaanisha kuwekwa huru, kufunguliwa kutoka katika gereza la vifungo
vya Ibilisi. Hata leo, unaposikia habari hizi, ukikubali kumpokea Yesu, vifungo
vyote alivyokufunga shetani, vitaisha muda huu ! ukikubali Yesu aingie
ndani ya ndoa yako, leo itakuwa shwari, matatizo yote yanaisha leo leo. Huo
ugonjwa hautavumilia kukaa ndani yako, unapompokea Yesu lazima uondoke, kwa
kuwa hauko gerezani tena, Yesu amechukua udhaifu wako wote.
Je, msalaba wa Yesu unamaana gani kwa kanisa la
leo ?
Msalaba wa Yesu ni ishara ya nguvu ya Mungu
itendayo kazi ;
Uwezo wa kuishinda dhambi tulionao, asili yake ni nguvu ya msalaba wa Yesu.
Uwezo wa kuacha pombe, kuacha sigara, ukahaba,umalaya, ugomvi, wizi, ujambazi,kulipiza
kisasi n.k. chanzo chake ni msalaba wa Yesu. Ni kupitia msalaba wa Yesu,wachawi
wameacha uchawi wao, walevi wameacha ulevi, wagomvi wameacha ugomvi,waliofungwa
na magonjwa wamewekwa huru, watu wamepata pumziko la kweli ndani ya Yesu.
Msalaba wa Yesu ni ishara ya kuwekwa huru ; Yesu alipowekwa msalabani,alibeba mizigo yako yote,
usikubali kung’ang’ania mzigo wo wote, mkabidhi Yesu, kama alivyokubali
kuchukua mashitaka ya Baraba, akakubali kuwekwa kwenye mti badala yake, hata
leo yuko tayari kuchukua mzigo wako ili uwekwe huru. Haiana haja ya kuendelea
kujitesa, mkabidhi hati ya mashitaka yako Yesu. Kumbuka Yesu alikuja kwaajili
yao waliopotea (Mathayo 9 :13) ili
awarejeshe kundini. Usikubali kuendelea kukaa nje ya zizi, njoo leo kwa Yesu
uwekwe huru. Kumbuka hati yako alisha iondoa, hukumu yako alishaibeba, kwanini
uendelee kukaa gerezani ? kumbuka Yeye
mwenyewe(Yesu) alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, …na kwa kuoigwa kwake, mliponywa (1Petro 2 :24).

Mambo gani yalitokea Baada ya Yesu kupandishwa
Msalabani ?
Pazia la hekaru lilipasuka ; hii inamaanisha ushindi mkubwa wa mkristo. Pazia kupasuka kunamaanisha
kuwekwa huru. Kuondolewa kwa vizuwizi vyote mbele yako.
Ikumbukwe kuwa, pazia,
liliwekwa kuwazuwia watu wasiingie wala hata wasiweze kupaona patakatufu pa
patakatifu. Mahali hapa,aliingia kuhani peke yake. Baada ya pazia kupasuka,
kizuwizi kiliondolewa kwa yeyote kufika hapo. Kifo cha Yesu msalabani,
kimeondoa dhambi zako, kimekupa kibali cha kunena kwa lugha kwa raha zako.
Tetemekeo kubwa; Tetemeko hili,liliambatana na giza nene,ikiwa ni ishara
ya nguvu kubwa yenye utisho wa ajabu sana. Tetemeko hili, lilionesha uwezo ulio
juu ya uwezo wote,nguvu inayozidi nguvu zote. tetemeko hili, lilidhihirisha
kuwa kweli Yesu ni mwana wa Mungu, na yule mlinzi alishuhudia kwa kinywa chake.
Hata leo, maisha ya mtu aliyeokoka, yanapaswa kudhihirika mbele za watu wote,
kuwa kweli kuna nguvu mpya na uweza wa ziada ndani ya mtu aliyeokoka.
Makabuli yalifunguliwa ; baada ya Yesu kushuka kuzimu, walio lala, wote wakaamka,
wakatangaziwa uzima upya. Wakawa katika uzima wa milele pamoja na Yesu ;
baada ya Yesu kumnyang’anya funguo za kuzimu ibilisi, akawa hana mamlaka tena,
uwezo wake wote na mamlaka yote akawa amenyeng’anywa. Nguvu ya msalaba, ni
nguvu inayoshinda mauti. Yesu ni zaidi ya mateso yote, ni zaidi ya kifo, ni
zaidi ya magonjwa, ni zaidi ya kukata tamaa, ni zaidi ya umasikini, nguvu ya
msalaba iko juu ya laana na vifungo vyote.
Tamko la Ushindi likatolewa ; tamko la ushindi lilitolewa rasmi Yesu aliposema (Imekwisha). Kauli ya
Yesu iliashilia kufikia mwisho kwa mateso yote, uonevu, laana, mikosi na
vifungo vyote. Kauli ya Yesu inatufundisha nini aliposema Imekwisha? Kwa
mtazamo wa ndani zaidi, ilimaanisha, kukamiliaka kwa kazi yake iliyomleta
duniani ambayo ilikuwa ni ukombozi. Kumweka
huru kila mtu ili asipotee, bali awe na uzima wa milele. Kwa
maelezo mengine tuseme kuwa, Msalaba wa Yesu, ulibadirisha Historia ya
Ulimwengu wote na kuweka utamaduni mpya.
Msamaha
wa dhambi ulitolewa;
kupitia mauti ya msalaba wa Yesu, msamaha wa dunia ulitangazwa. Kupitia kifo
cha msalaba, toba kwa ulimwengu ilipatikana. Kifo cha msalabani, kinatupa maji
ya uzima, kinatupa pumziko la kweli, kina tuhesabia haki. Wakati wayahudi
walidhani wanakomesha, kumbe agano la Mungu linatimia kwa ulimwengu, kuwa Mtu
hatafika mbinguni ila kwa njia ya Yesu Kristo. Kupitia kifo cha Yesu, mlango wa
kuiendea mbingu ilifunguliwa wazi kwa wote wampokeao na makao yao yakaanza
kuandaliwa tangu hapo. Hata leo, ukiokoka, makao yako yanaanza kuandaliwa leo.
MAOMBI

Ndugu yangu,
natumai umesoma ujumbe huu, leo Roho wa Mungu amenituma kwako, nikuueleze
habari hii ya Msalaba, sijui umeteseka kwa kiwango gani katika hali hiyo
uliyonayo, wala sijui hamu yako ya kumtumikia Mungu inalinganaje, wala sifahamu
umesongwa kwa kiwango gani, pengine umefikia hatua ya kukata tamaa, huoni
msaada utatoka wapi, lakini ujumbe huu umefika kwako muda huu; upo msaada
usioisha,upo uweza usioshindwa, ipo nguvu isiyoteteleka, nayo ni nguvu ya Msalaba
wa Yesu Kristo, aliye chukua laana na uovu wetu ili tupate kuwa huru.
Aliyechukua dhambi zetu, aliyebeba magonjwa yetu, huzuni zetu na kila adha;
unapo pata habari hizi, nakusihi sana usikubali kuendelea kukaa katika vifungo
hivyo, toka gerezani, Mungu amekukumbuka, amekuona,usifanye moyo wako kuwa
mgumu, jiachilie kwake uwe huru, kwa Jina la Yesu Kristo. Pokea kwa kadri ya
uhitaji wako, unayetaka mwenza, unayetaka mtoto, unayetaka kuinuliwa katika
masomo, usiye na kazi, unayeteswa na madeni, kila kona unavutwa shati, kwa Jina
la Yesu, unayeonewa kazini kwako, umeshushwa cheo, umeonewa vya kutosha, kwa
Jina la Yesu, pokea uweza mpya na nguvu mpya. Uwe huru sasa, ufurahi tena,
ububujike amani tele moyoni, kwa Jina la Yesu Kristo.
Kama unahitaji
kuokoka, au ungependa kupata ushauri wowote maombezi au kutoa ushuhuda,
wasiliana na


Mwl. Sospeter
Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.
Kwa Mobile +255(0)7
(57/84) 464 141/ 12 909 021.
Tunakushauri,
utembelee kanisa la kiroho lililo jirani yako, kwaajili ya mafundisho zaidi na
Ushirika. (Kumbukumbu la Torati 28:6).
![]() |
No comments:
Post a Comment