Bwana Yesu asifiwe sana.
Namshukuru Mungu kwaajili yako unaesoma
ujembe huu-Mungu akubariki sana na kukuepusha na balaa zote,afute laana na
mikosi inayokuzunguka katika jina la Yesu Kristo.
Ndugu yangu, naomba nikukaribishe katika
somo letu la leo:
MADA
KUU: KUDUMU KATIKA MAOMBI.
Kwanza Kabisa,naomba kukueleza kwaufupi
sana kuwa Dhana ya "kuomba" ni
kuwasilisha mahitaji ili upatiwe msaada.
Aidha, kwa muktadha huu, kuomba ni
kuwasiliana na Mungu ambaye ndiye baba yetu na mwokozi wa maisha yetu-Haleluya!
(A)Maandalizi kabla ya kuanza Kuomba.
(i) Hakikisha Moyo wako ni safi mbele za
Mungu, usiwe na kinyongo,hasira wala mwenye mawazo mabaya, hivyo jitakase
kwanza kabla ya kuanza maombi.Zaburi
29:2b...mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu
(ii) Tubu ili utakaswe hata Mungu
akusikilize,omba rehema za Mungu ziwe juu yako ndipo uanze kuomba Isaya 1:18.
(B)Namna ya kuomba.
(i) Kwanza maombi ni lazima ujue unaomba
nini na kwa nani.
Yesu alisema, na lolote mtakaloomba kwa
Baba yangu, ombeni kwa jina Langu,tena akasema, na lolote mtakaloomba kwa jina
langu, mmeshapata.
Hivyo, yakupasa kuomba kwa usahihi,kupitia
Jina la Yesu kwa kuwa ndilo jina pekee tulilopewa wanadamu kuolewa kwalo....na
zaidi hili ndilo jina kuu kuliko majina yote Wafilipi 2:10-11
Maana yake ni kuwa,kuomba kwa kupitia jina
lingine ni sawa na kukosea namba za unaempigia simu,je unataegemea kumpata
unayempigia simu?
Kwa ufupi. usalipo usizunguke,piga moja kwa
moja kwa Yesu naye atatenda hapo hapo.
(ii) Jenga Imani ya kuwa Mungu hashindwi wala si kigeugeu,kila
uombacho sharti upate kwa mapenzi yake. Mathayo 7:7,tena kuwa thabiti katika
maombi yako hata kwa kufunga Mathayo 17:20-21.
(iii) Kuwa na msatari wa kusimamia katika
maombi yako,kwa kuwa Bwana anasema leteni hoja zenye nguvu, tena anaongeza
"unikumbushe na tuhojiane....Isaya 43:26,BWANA anakuona na yuko tayari
kukuhudumia endapo utachukua hatua ya kuomba kwa imani Yeremia 29:11-12
(iv) Kuwa tayari kwa matokeo yoyote
ilimradi yameamriwa na Mungu yatokee,Shukuruni kwa kila jambo,na kila jambo na
wakati wake,usilazimishe Mungu afanye vile unataka,yaache yaliyomapenzi yake
yatimie Mathayo 7:10,pia Muhubiri 3:1.
(C)Mwisho wa Maombi.
Hitimisha kwa kushangilia kwa kuwa Mungu
ameyasikia maombi yako na yuko tayari kufanya vile anavyoona inafaa.
Jitakase tena,omba ulinzi wa Roho
mtakatifu,soma biblia,endelea kukua katika hali ya kumpenda Mungu na Utamani
zaidi kujifunza mengi kutoka kwake.Mungu akubariki,akuinue na ukupe muujiza
wake katika jina la Yesu Kristo.
Amen
No comments:
Post a Comment