Translate
Friday, June 28, 2013
SOMO: JIFUNZE KUFUMBA MACHO.
Lengo kuu: Kuacha Dhambi.
Lengo Mahususi: Kila mtu,kuacha Dhambi na kuwa mwanafunzi wa Yesu, kumpenda Mungu peke yake, na kuziacha njia nyingine.
Utangulizi.
Ndugu zangu, napenda niwakaribishe katika somo letu fupi sana, ambalo kwa hakika, nina imani Mungu hatakuacha umalize kusoma ujumbe huu, bila kukuhudumia. Na wala, hata acha kukulipa muda huu, unaoutumia kujifunza maneno haya, hata ukaacha kufanya kazi nyingine, na kuuachilia mwili,fikra na mawazo hata pesa yako, ili uweze kusoma ujumbe huu; Mungu akubariki sana.
Napenda kukushirikisha juu ya haya hili neno “Kufumba Macho”
Ni wazi kuwa, kila mara, katika maeneo mbali mbali, huwa tunafumba macho mara tunapotaka kuomba”haleluya”. Utaratibu huu, ambao umefanywa kuwa kanuni, mara zote hufanywa kwa lengo la kuvuta umakini na hisia kwa Mungu. Njia hii, humfanya mtu, atulie kimawazo na hata kiakili. Kwa kujitenga na ulimwengu na mambo yanayopita katika upeo wa macho yake.
Aidha, kufunga macho humfanya mtu, asibugudhiwe na vitu vinavyopita mbele yake, ambavyo vinaweza kumhamisha kimawazo, na kumfanya ashindwe kuomba vizuri. Wakati mwingine, inapotokea kitu cha kutisha, mtu hufumba macho, ili asiendelee kuona kicho kitu kinachokuja mbele yake, ambacho pengine kitamtoa katika msimamo wake.
A. JE, KUFUMBA MACHO MAANA YAKE NI NINI HASA?
****Kiimani, kufumba macho, ni zaidi ya kuacha kuona, kwa maana hata kipofu, haoni ila anaweza akawa hajafumba macho. Kufumba macho, ni hali ya “kuacha dhambi” na kuamua kuiacha kabisa, na kumtafuta Mungu. Kumwangalia Mungu tu.
****Kuokoka, ni kufumba macho; kuamua kujikabidhi kwa Mungu, siyo suala la mchezo, kwani mwanadamu anapookoka, wakati jina lake linaandikwa katika kitabu cha uzima, hata kuzimu huandikwa kwa kuwa ametangaza vita na shetani. Si maanishi kuwa mtu asiokoke, eti kwa kuogopa kuwa katika vita na shetani, la hasha! Ndiyo maana biblia inasema, “je, twendelee kutenda dhambi kwa kuwa neema ipo, hasha” lakini pia, kumbuka pia, ahadi za Mungu kwetu kuwa, “hii vita tunayopigana si ya kwetu, bali ni yake yeye mwenyewe”(2Nyakati 20:15), tena, imetupasa, kumwamini yeye kwakuwa, yu na nguvu zaidi ya huyo adui yetu (Kutoka 14:13, Kumb1:29&30, 2Nyakati 32:7).
****Kuacha dhambi, ni kufumba macho” ebu fikria, mwanadamu ambaye kiasili, anaishi kwa kuiba, kutapeli, kufanya ukahaba, kunyang’anaya n.k. mtu huyu, ameifanya dhambi kuwa sehemu yake ya kutafutia maisha, kuacha kazi hiyo si jambo la masihala, ni jambo linalihitaji ujasiri. Inahitaji nguvu ya Mungu, na hapo ndipo tunapoomba Mungu sana atusaidie.
****Kuacha ulevi, ni kufumba macho, mtu aliyezowea kunywa pombe, kuvuta sigara, bangi na vileo vinginevyo, kuviacha si mchezo. Mtu aliye athiriwa na madawa ya kulevya, kuyaancha mpaka nguvu ya Mungu imshukie.
****Kuacha uchawi, ni kufumba macho, kwa hali ya kawaida, mwanadamu aliyeweka tumaini juu ya nguvu za kipepo, kuziacha huwa ni vigumu sana, kwa kuwa, huyo ndiye mungu wake, anayemtumikia, hata hivyo kumchomoa katika imani hiyo, si jambo la lelemama, inahitaji uweza wa Mungu.
****kuacha umbeya, kuseng’enyana ni kufumba macho. Mtu aliyezowea kusemana wenzie, hata akilala, huota anasutana, huota anamsema mwenzake, hata akiwa anahubili, atatoa mifano inayowahusu wengine, si kwa lengo la kujenga, bali kubomoa, mwanadamu mwenye tabia hii, kuacha tabia hii, inahitaji nguvu ya Mungu.
***Kumpenda mke/mme wako kwa dhati ni kufumba macho, suala la kupenda, ni suala amabalo lipo kila siku na halijafungiwa kikomo, hivyo, mtu kumpenda mke/ mme wake kwa dhati, kama ilivyoamuliwa ni kufumba macho. Kutokuwaona hao ma”handsome” na ma“beautiful” wapya, kuwaacha madogodogo, maserengeti boys, ni kufumba macho.
B. KUMTUMIKIA MUNGU NI KUFUMBA MACHO?
****Lakini, ndugu msomaji, inabidi ujue kuwa, kumtumikia Mungu pia ni kufumba macho, kumtii na kuzishika amri zake, ni kufumba ,macho, wala siyo kwamba na kutisha, lazima ifike mahali ujuwe kuwa, unapoamua kumtumikia Mungu, si suala la kulala na kuamka, kama unavyoweza kuamua kujenga banda la kuku; Yesu mwenyewe alisema; “kama unataka kunifuata mimi, sharti, ujikane, ujitwike msalaba ndipo umfuate” tena akasema, unapaswa kuhesabu gharama halisi” na ukimfuata, sharti, usiwe wa kugeuka geuka nyuma. Tena anasema, hapendezwi nao wenye nia mbili. Kuna wakati, unapita katika majaribu,ndugu wanakutenga na pengine unabaki peke yako, hata mimi nimepita katika hali hizo, lakini inakupasa uwe na ujasiri, usimamie iliyo kweli daima, hata kama unauma. “Kuwa tayari, kuvumilia uchungu wa ukweli, kuliko kufurahia, utamu wa Uongo”. Na hapa ndipo Joshua aliposimama na kutangaza hadharani” ….lakini Mimi pamoja na nyumba yangu, tutamtumikia Bwana” (Yoshua 24:15)
****Kutii sauti ya Mungu, ni kufumba macho, Kumbuka kuwa, wakati Mungu anatoa maelekezo juu ya njia unayopaswa kuiendea, shetani pia, huingilia kati na kutoa maelekeza yake, mara zote, shetani hitoa maelekezo yanayofaa machoni pa mwanadam, hulaghai kwa sauti nyololo na kukuonesha mambo mazuri na matamu. Angalia nyoka alivyomdanga Hawa na kuyaacha maagizo ya Mungu, akayaangalia matunda yapendezayo mtini, na kuyala (Mwanzo 3:1-7). Lakini, hata Yesu mwenyewe alidanganywa na Ibilisi mara kibao, ashukuriwe aliyejuu, Yesu, hakuangalia mkate wala miliki za dunia, alifumba macho na kuiangalia mbingu mpaka mwisho.
****Kutoa sadaka nikufumba macho! Maandiko matakatifu, yanatueleza juu ya kumtolea Mungu sehemu zilizo nona, na kupitia matoleo yetu,ndipo Baraka hufunguliwa kwetu. Hata hivyo, imekuwa ngumu kulitii andiko hili, ndiyo maana, ni vigumu kwetu kumtolea Mungu matoleo mazuri, badala yake tunatoa masalia. Haikuwa lahisi kwa Ibrahim kumtoa Isaka, huku anajua ndiye mwanae wa pekee na mrithi wake. Isipokuwa, ilimpasa afumbe macho, na hapo ndipo alipobarikiwa (Mwanzo 22:1-15)
****Kuitii sauti ya Mungu mpaka mwisho, nikufumba macho, ndiyo maana mtu hupita katika majaribu makubwa na mazito, magumu na ya kutisha ila unapaswa kufumba macho, kumbuka neno la Mungu linasema “atakayevumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka” hata wewe unapaswa kuvumilia mpaka, mwisho,usione hatari hata kufa kwa kuisimamia kweli, kwanini udanganye, au umkane Yesu kwa kitu kidogo, leo mtu yuko tayari kubadiri dini kwasababu ya ndoa tu, kwanini unaufanya ukristo kuwa bei chee kiasi hiki. Akina Meshaki, Shadraki na Abednego, wako wapi leo, watu waliokubali kufa kwaajili ya Mungu. Watu wenye imani kama Elia, leo wako wapi?
Pengine Muda unaweza usitutoshe kumaliza somo letu, kama umebarikiwa, uweze kushare ujumbe huu, ili kuifanya kazi ya Mungu, usishangae ukiona watu hawacomment, pengine wameamua kuufanyia kazi ujumbe huu kimya kimya. Mungu akubariki sana.
Na.
Mwl. Sospeter Simon S. Ndabagoye
New Elshaddai Ministrie NEM-Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment