Translate

Tuesday, June 25, 2013

TAFAKARI YA JIONI

Tazama mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili;Je! kuna neno gani gumu nisiloliweza? (Yeremia 32:27).

Tazama yaani kuwa makini, tafakari,tuliza Bongo!Fanya tathmini

Mimi ni BWANA- yuko juu ya wote, ndiye mtawala mkuu!Wengine wote watumishi tu!

Mungu wa wote wenye mwili- Yaani Mwabudiwa na wote wenye mwili!

Je!- Haya sasa, linganisha, tena kwa kushangaa, nani mwingine, hapa nisawa na kulindanisha Piki piki ya miti na Range, kwenye mlima.Lazima tushangae wote.

kuna neno gumu lolote- Kuna jambo liwalo lote?Fikiri kwa Kina tafadhari, pima shida yako, anagalia hitaji lako? Lile unaloona kuwa limeshindikana kwako. Pengine ni ugonjwa, umedharauliwa, umetengwa na ndugu, umekosa mme/mke, huna watoto wakati unasitahili kuwa nao, umefukuzwa kazi. n.k.

Nisiloliweza? Linganisha sasa, tatizo lako na uwezo wa Mungu.Je tatizo lako ni kubwa sana kumshinda Mungu?

Kumbuka hili: Waakati Jeshi lote la Israeli, lilimwona Goriathi, pande la Baba lisolowezekana, Daudi, alimwona ndiye mzuri kulenda shabaha, kwa kuwa kwenye mwili wote huo, hatakosa pa kupiga!Haleluya, hata wewe siku ya leo nataka ujue hili, Kadri Tatizo linavyozidi kuwa kubwa, na ukazidi kulikabili kwa kumtegemea Mungu, undivyo Yesu anavyojisogeza kwako. Kumbuka Meshaki, Shadrack na Abedinego, walipotupwa kwenye Tanuru la Moto, ndipo Yesu aliposhuka!(Daniel 3:25) Hata leo yupo tayari kukuokoa na hatari uliyo nayo kama utamwamini na kumlilia tena kwa Ujasiri.Yesu yuko tayari kulivaa tatizo lako, kama ukimtumaini.

ENDELEENI KUBARIKIWA


No comments:

Post a Comment