Translate

Thursday, December 26, 2013

SIKU KUU YA KRISMASI.

Utangulizi.

Dhana ya Jina la Krismasi.
Neno krismasi, linatokana na maneno mawili, Kris(Kristo) linalo maanisha masihi wa Bwana, yaani mpakwa mafuta wa Bwana. Masi(mass) likimaniisha kusanyiko; hivyo dhana Krismasi ni kusanyiko la wakristo, au kusanyiko kwaajili ya kristo. Epukana na dhana nyingine zisizofaa kama vile XMASS- ambayo huweza kupotosha maana halisi. Kumbaka kuwa hakuna krismasi bila Kristo, kwa hiyo neno XMASS ni neno linaloweza kuwa na dhana kamili iliyotofauti na Krismasi.

Asili ya krismasi.
Wazo la Krismasi liliasisiwa na Mungu mwenyewe alipokuwa akipanga mbinu ya ukombozi baada ya dhambi kumtenga mwanadamu na Mungu wake. Hivyo Mungu akauweka mpango makili wa ukombozi. (Rumi 5:12, Efeso 2:1-3).

Swali la kujiuliza ni je, kama Mungu alijua kuwa kupitia Mariamu ulimwengu utakombolewa, kwanini hakumwona kuwa anatosha yeye mwenyewe peke yake kuukomboa ulimwengu?

Huku tukiendelea kujiuliza vichwani mwetu, tutabaini kuwa, licha ya Mungu kumuumba mwanadamu na kumpa mamlaka ya kurithi na kutawala na kutisha, lakini ibilisi aliweza kumwangusha; hivyo ikambidi aweke mkakati maalum kutoka mbinguni kwa kuwa hata asili ya shetani ni mbinguni japo hawezi kurudi kamwe, hivyo Mungu akamleta mwanae wa pekee kutoka huko(mbinguni) ili aje na kuukomboa ulimwengu dhidi ya utumwa wa dhambi.
Hivyo, Yesu alikuja na kuishi kwetu kama mwanadamu japo alikuwa Mungu kamili.(Luka 1:26-35). Alikuwepo tangu asili hata kabla ya ulimwengu kuwako.(Yohana 1:1,3&14).

Je kusudi la yesu kuja duniani ni nini?

Kuna sababu kadha wa kadha za ujio wa Yesu, zifuatazo ni baadhi tu ya sababu kuu za ujio wake.

(a) Kutukomboa wanadamu.
Ili kumtoa mwanadam chini ya utumwa wa dhambi na utawala wa shetani. Mwanadam alianza kuishi chini ya utawala huu, tangu alipokubali kuitii sauti ya ibilisi na umtenda Mungu dhambi kwa kula tunda alilokatazwa,hivyo, mwanadam alipoisikia sauti ya ibilisi, tayari alivunja uhusiano wake na Mungu.
Kwa kigezo hicho, ujio wa Yesu ni kwaajili ya kututoa mateka (Kolosai 1:13, Luka 19:10) chini ya udhibiti wa joka la zamani, mwenye gadhabu audanganye ulimwengu.

(b) Kurejesha Ushirika wetu na Mungu.
Baada ya dhambi kuingia ulimwenguni, mwanadamu aliungana na ibilisi na kuwa mali yake (1Yohana 1:3), mpaka Mungu alipomtuma Yesu aje kumrejesha upya. Hivyo, kazi kuu ya Yesu ilikuwa kuurudisha uhusiano ulioporwa na shetani (the lost opportunity).
Kwa hiyo, ujio wa Yesu umemweka mwanadamu katika familia ya Mungu. (Yohana 1:12, 1Yahana 3:1&2).

(c) Kutununua.
Yesu alifanyika fidia kwa kuutoa uhai wake msalabani (Mathayo 20:28), kwa kigezo hicho, damu na maji ya Yesu, vilifanyika toba ya kweli na msamaha kwa ulimwengu na kuwa patanisho la milele na Mungu.
Kupitia kifo cha msalaba, mwanadamu aliyekuwa chini ya utumwa na umiliki wa ibilisi, simba aungurumae mchana/ chatu mwenye njaa na gadhabu nyingi alipata tumaini jipya la uzima wa milele kwa kuwekwa huru na kutengwa na dhambi(1Yohana 5:11&12, Yohana 3:16&17, 10:10).

(d) Kututenga mbali za kazi za shetani.
Yesu alikuja kuvunja na kuharibu kazi za mfalme wa giza alie ibilisi(1Yohana 3:8). Ifahamikie kuwa, mwanadamu alipoacha kumtumikia Mungu, basi alianza kumtumikia shetani, hivyo Yesu alikuja kuvunja mkataba huo na ndiyo maana aligharimia mkataba huo kwa damu yake.

(e) Ili kuwani ishara ya upendo wa Mungu kwa mwanadamu (1Yohana 4:9&10,Rumi 5:8)
Yesu alikuja kwaajili ya watu wote, na aliwakomboa kwa pamoja, bila kujali sura, asili, mali n.k. hivyo, ili kuonesha upendo wake wa dhati, ilimbidi ashuke chini na anyeneyekee hadi kifo cha msalaba.
HITIMISHO.
Hatahivyo, Mungu alipanga kuonesha uwezo wake na nguvu zake kuwa ziko juu zaidi. Ndiyo maana, ujio wa Yesu ulimabatana na kuzibatilisha kazi za ibilisi zikimabatana na miujiza (Yoha 6:1-21, Marko 4:37-41),Uponyaji (Mathayo 4:24,Yohana 9:1-7),Utoaji wa pepo na kufungua vifungo vyote (Marko 1:34, 5:1-7,) hata kufufua waliokufa tayari (Yohana 11:43&44). Hili lilienga kutoa mamlaka kuu zaidi kwa watao mwamini ili watende haya na zaidi ya haya. Haleluyaaaaaaaa.
New Elshaddai Minisries NEM-Tanzania inawatakia Kila la Kheri, muwe na siki kuu njema, iliyojaa amani, upendo na furaha.
Mungu awabariki sana.
Na. Mwl. Sospeter Simon S. Ndabagoye.

Saturday, August 24, 2013

KUDUMU KATIKA MAOMBI

Bwana Yesu asifiwe sana.

Namshukuru Mungu kwaajili yako unaesoma ujembe huu-Mungu akubariki sana na kukuepusha na balaa zote,afute laana na mikosi inayokuzunguka katika jina la Yesu Kristo.

Ndugu yangu, naomba nikukaribishe katika somo letu la leo:

 MADA KUU: KUDUMU KATIKA MAOMBI.

Kwanza Kabisa,naomba kukueleza kwaufupi sana kuwa Dhana ya  "kuomba" ni kuwasilisha mahitaji ili upatiwe msaada.
Aidha, kwa muktadha huu, kuomba ni kuwasiliana na Mungu ambaye ndiye baba yetu na mwokozi wa maisha yetu-Haleluya!

(A)Maandalizi kabla ya kuanza Kuomba.

(i) Hakikisha Moyo wako ni safi mbele za Mungu, usiwe na kinyongo,hasira wala mwenye mawazo mabaya, hivyo jitakase kwanza kabla ya kuanza maombi.Zaburi  29:2b...mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu
(ii) Tubu ili utakaswe hata Mungu akusikilize,omba rehema za Mungu ziwe juu yako ndipo uanze kuomba Isaya 1:18.

(B)Namna ya kuomba.

(i) Kwanza maombi ni lazima ujue unaomba nini na kwa nani.
Yesu alisema, na lolote mtakaloomba kwa Baba yangu, ombeni kwa jina Langu,tena akasema, na lolote mtakaloomba kwa jina langu, mmeshapata.
Hivyo, yakupasa kuomba kwa usahihi,kupitia Jina la Yesu kwa kuwa ndilo jina pekee tulilopewa wanadamu kuolewa kwalo....na zaidi hili ndilo jina kuu kuliko majina yote Wafilipi 2:10-11
Maana yake ni kuwa,kuomba kwa kupitia jina lingine ni sawa na kukosea namba za unaempigia simu,je unataegemea kumpata unayempigia simu?
Kwa ufupi. usalipo usizunguke,piga moja kwa moja kwa Yesu naye atatenda hapo hapo.
(ii) Jenga Imani  ya kuwa Mungu hashindwi wala si kigeugeu,kila uombacho sharti upate kwa mapenzi yake. Mathayo 7:7,tena kuwa thabiti katika maombi yako hata kwa kufunga Mathayo 17:20-21.
(iii) Kuwa na msatari wa kusimamia katika maombi yako,kwa kuwa Bwana anasema leteni hoja zenye nguvu, tena anaongeza "unikumbushe na tuhojiane....Isaya 43:26,BWANA anakuona na yuko tayari kukuhudumia endapo utachukua hatua ya kuomba kwa imani Yeremia  29:11-12
(iv) Kuwa tayari kwa matokeo yoyote ilimradi yameamriwa na Mungu yatokee,Shukuruni kwa kila jambo,na kila jambo na wakati wake,usilazimishe Mungu afanye vile unataka,yaache yaliyomapenzi yake yatimie Mathayo 7:10,pia Muhubiri 3:1.

(C)Mwisho wa Maombi.
Hitimisha kwa kushangilia kwa kuwa Mungu ameyasikia maombi yako na yuko tayari kufanya vile anavyoona inafaa.

Jitakase tena,omba ulinzi wa Roho mtakatifu,soma biblia,endelea kukua katika hali ya kumpenda Mungu na Utamani zaidi kujifunza mengi kutoka kwake.Mungu akubariki,akuinue na ukupe muujiza wake katika jina la Yesu Kristo.

Amen

MSALABA

MSALABA

Lengo kuu: Kujua Maana, Sababu na Nguvu ya Msalaba.
Lengo Mahsusi: Kila Mkristo kujua uwezo ulio ndani ya msalaba.

Swali: Msalaba unaweza kukukinga na mashambulizi ya shetani?
Nini maana ya Msalaba?
 600638_316706671752858_748566843_n.jpg

Dhana ya Msalaba,inafasiliwa kwa utofauti kulingana na mtazamo wa jamii hiyo na pengine mapokeo yao. Hivyo, maana ya msalaba,hutegemea na wakati na mazingira. Kwa dhana hii, hatuwezi kupata maana moja ilinayounganisha jamii zote na nyakati zote.
Zifuatazo ni baadhi ya fasili za Msalaba:
Uamuzi mgumu :- maana hii ilitolewa na Yesu mwenyewe katika (Luka 14 :17) ikimaanisha gharama kubwa sana, ambayo ni sharti  mtu atulie na kuitafakari kwa kina. Hii inatupa kujifunza kuwa, kuuchukua msalaba si suala la mchezo, ni suala linalohitaji maandalizi. Pengine niweke wazi kuwa, wokovu, si kitu cha kukurupuka, wala kuigiza, bali yakupasa kujitafakari kwa kina na kuchukua uamuzi moyoni mwako kwa kumaanisha.
Msalaba ni Laana :- Wayahudi waliamini kuwa, msalaba ni ishara ya kukataliwa katika jamii yote. Yaani, kutokukubalika katika jamii. Na kifo cha msalabani, ni kifo cha aibu sana mapochoni pao. Msalaba ni ishara ya kutokufaa katika jamii yote. Kifo hiki cha msalabani, alihukumiwa mtu asiyefaa kabisa kwa kiwango cha juu kabisa. Ni kifo kilicho dharauliwa kuliko hata mbwa. Ni kifo cha kudharirisha alichositahiri mtu aliyekithiri kwa uovu wake katika jamii yote. Pengine kifo hiki, kilifanyika kwaajili ya kukomesha tabia ya aliyehukumiwa. Kama ni mwizi, basi ilifanyika hivi ili kukomesha wizi, na kama ni mchawi, kwaajili ya kukomesha uchawi. Kwa maelezo hayo, tunang’amua kuwa, kifo cha Yesu Msalabani,kililenga kukomesha Ukristo (tabia za Kristo) duniani. Maana yake, ni kutokukubaliana na kile alichokuwa akitenda duniani. Na kwa hatua hii, ni laana kwake na kwa wafuasi wake wote. Pia, hii iliachilia mlango wazi kutendewa hivi yeyote atakayeonekana, kumfuata Yesu.
 Kubeba mzigo mzito sana :- jamii nyingi, hata fasili aliyotoa Yesu utabaini kuwa, msalaba, unahusishwa na mzigo mzito sana,ambao hayubebeki, mzigo ambao kwa hali ya kawaida,hauwezekani,isipokuwa unalazimika kuubeba. Ijulikane kuwa, hata Yesu, kuna kipindi alifikia hatua ya kutokutaka kuubeba msalaba, isipokuwa kwa mapenzi ya Baba tu, ndipo aubebe(Mahayo 26 :42). Kwa mtazamo huo, tunabaini kuwa ni dhahiri, kwa wakati ule na mazingira yale, msalaba ulikuwa na maana hiyo kwa jamii hiyo.
Kwamaana hiyo swali lakujiuliza ni je, kama huo ndio ukweli wake, inakuwaje, mtu anavaa msalaba, na pengine hata kwenye kaburi unakuta umewekwa msalaba ? Inamaana, mtu anaaamua kubeba mzigo wake mwenyewe siku zote ?  au ndugu wa marehemu wanamtwika ndugu zao mzigo ? Lazima jibu liende mbali ya hapo zaidi.
Ukweli ni kuwa, pamoja na dhana hizo zote, kuwa msalaba ni laana, msalaba ni mzigo mzito,msalaba ni uamzi usio wa kawaida, kwa ulimwengu wa leo, Msalaba ni Ukombozi, Msalaba ni Ushindi, Msalaba ni kuwekwa Huru. Kwa fasili hii, tunapata maana moja,inayounganisha jamii zote, maeneo yote na nyakati zote na tamaduni zote. Na hii ndiyo sababu, unakuta mtu amevaa msalaba,mwingine amepamba kwenye nyumba yake, au kwenye gari amechora msalaba. Hata kwenye kaburi, anaweka msalaba, japo wengine wanafanya hivyo tuu, kama ishara ya dhehebu flani, au kinga ili wasivamiwe na mapepo, ila ukweli unabakia kuwa wazi kwamba, msalaba wa kweli, unaanzia rohoni wala si vazi au urembo flani.
…akisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu,akaiondoa isiwepo tena,akaigongomea msalabani (Wakolosai 2 :14). Kupitia kifo cha Yesu msalabani, tunapata kuona kuwa, hati yetu ya mashitaka iliondolewa, tuliwekwa huru. Mashitaka yetu,yaligomgomewa msalabani. Dhambi zetu, zilichukuliwa pale msalabani, kifo cha Yesu msalabani,kilipelekea ulimwengu kuhesabiwa haki.523228_10150620208771431_1592957770_n.jpg
Kwanini Yesu alikufa msalabani wala si kifo kinginecho ?
Pamoja na Yesu kuja kwetu kwa upendo, kwa wema mwingi, akafanya miujiza mingi lakini kwa wayahudi,bado alionekana hafai,pamoja na kuwaponya ndugu zao,pamoja na kuwafufua ndugu zao waliokufa, lakini bado, walimwona hafai, wakamkataa. Hata Pilato alipouliza, kati ya Yesu na Baraba, afunguliwe nani ; wakapaza sauti zao kwa pamoja ‘ afunguliwe Baraba’ hii inamaana kuwa, walimkataa Yesu,wakamkubali Baraba, wakamwona Baraba ni bora kuliko Yesu.
Nia ya wayahudi,ilikuwa kummaliza kabisa Yesu na kufuta Historia yake kabisa kwenye ulimwengu watu waliowahi kutenda jambo lolote jema. Walilenga kuanzisha Historia mpya juu yake, endapo atakumbukwa, basi akumbukwe kwa uovu wala si kwa wema. Kumbe mawazo ya Mungu, si ya mwanadamu, nia ya Mungu, na njia zake hakika hazichunguziki, ukuu wake ni wa ajabu mno; na mawazo yake si sawa na mawazo ya binadamu. Nia ya Mungu  ilikuwa kumkomboa mwanadamu, ilikuwa kumweka huru aliyefungwa. Baada ya Yesu kukamatwa, hati mauti ya msalaba ya Baraba, ikafutwa mara moja.
Kuachiliwa kwa Baraba kulimaanisha kuwekwa huru, kufunguliwa kutoka katika gereza la vifungo vya Ibilisi. Hata leo, unaposikia habari hizi, ukikubali kumpokea Yesu, vifungo vyote alivyokufunga shetani, vitaisha muda huu ! ukikubali Yesu aingie ndani ya ndoa yako, leo itakuwa shwari, matatizo yote yanaisha leo leo. Huo ugonjwa hautavumilia kukaa ndani yako, unapompokea Yesu lazima uondoke, kwa kuwa hauko gerezani tena, Yesu amechukua udhaifu wako wote.
Je, msalaba wa Yesu unamaana gani kwa kanisa la leo ?
Msalaba wa Yesu ni ishara ya nguvu ya Mungu itendayo kazi ; Uwezo wa kuishinda dhambi tulionao, asili yake ni nguvu ya msalaba wa Yesu. Uwezo wa kuacha pombe, kuacha sigara, ukahaba,umalaya, ugomvi, wizi, ujambazi,kulipiza kisasi n.k. chanzo chake ni msalaba wa Yesu. Ni kupitia msalaba wa Yesu,wachawi wameacha uchawi wao, walevi wameacha ulevi, wagomvi wameacha ugomvi,waliofungwa na magonjwa wamewekwa huru, watu wamepata pumziko la kweli ndani ya Yesu.
Msalaba wa Yesu ni ishara ya kuwekwa huru ; Yesu alipowekwa msalabani,alibeba mizigo yako yote, usikubali kung’ang’ania mzigo wo wote, mkabidhi Yesu, kama alivyokubali kuchukua mashitaka ya Baraba, akakubali kuwekwa kwenye mti badala yake, hata leo yuko tayari kuchukua mzigo wako ili uwekwe huru. Haiana haja ya kuendelea kujitesa, mkabidhi hati ya mashitaka yako Yesu. Kumbuka Yesu alikuja kwaajili yao waliopotea (Mathayo 9 :13) ili awarejeshe kundini. Usikubali kuendelea kukaa nje ya zizi, njoo leo kwa Yesu uwekwe huru. Kumbuka hati yako alisha iondoa, hukumu yako alishaibeba, kwanini uendelee kukaa gerezani ? kumbuka Yeye mwenyewe(Yesu) alizichukua dhambi zetu katika mwili wake  juu ya mti, …na kwa kuoigwa kwake, mliponywa (1Petro 2 :24).

Sospeter.JPG

Mambo gani yalitokea Baada ya Yesu kupandishwa Msalabani ?
Pazia la hekaru lilipasuka ;  hii inamaanisha ushindi mkubwa wa mkristo. Pazia kupasuka kunamaanisha kuwekwa huru. Kuondolewa kwa vizuwizi vyote mbele yako.
Ikumbukwe kuwa, pazia, liliwekwa kuwazuwia watu wasiingie wala hata wasiweze kupaona patakatufu pa patakatifu. Mahali hapa,aliingia kuhani peke yake. Baada ya pazia kupasuka, kizuwizi kiliondolewa kwa yeyote kufika hapo. Kifo cha Yesu msalabani, kimeondoa dhambi zako, kimekupa kibali cha kunena kwa lugha kwa raha zako.
Tetemekeo kubwa; Tetemeko hili,liliambatana na giza nene,ikiwa ni ishara ya nguvu kubwa yenye utisho wa ajabu sana. Tetemeko hili, lilionesha uwezo ulio juu ya uwezo wote,nguvu inayozidi nguvu zote. tetemeko hili, lilidhihirisha kuwa kweli Yesu ni mwana wa Mungu, na yule mlinzi alishuhudia kwa kinywa chake. Hata leo, maisha ya mtu aliyeokoka, yanapaswa kudhihirika mbele za watu wote, kuwa kweli kuna nguvu mpya na uweza wa ziada ndani ya mtu aliyeokoka.
Makabuli yalifunguliwa ; baada ya Yesu kushuka kuzimu, walio lala, wote wakaamka, wakatangaziwa uzima upya. Wakawa katika uzima wa milele pamoja na Yesu ; baada ya Yesu kumnyang’anya funguo za kuzimu ibilisi, akawa hana mamlaka tena, uwezo wake wote na mamlaka yote akawa amenyeng’anywa. Nguvu ya msalaba, ni nguvu inayoshinda mauti. Yesu ni zaidi ya mateso yote, ni zaidi ya kifo, ni zaidi ya magonjwa, ni zaidi ya kukata tamaa, ni zaidi ya umasikini, nguvu ya msalaba iko juu ya laana na vifungo vyote.
Tamko la Ushindi likatolewa ; tamko la ushindi lilitolewa rasmi Yesu aliposema (Imekwisha). Kauli ya Yesu iliashilia kufikia mwisho kwa mateso yote, uonevu, laana, mikosi na vifungo vyote. Kauli ya Yesu inatufundisha nini  aliposema Imekwisha? Kwa mtazamo wa ndani zaidi, ilimaanisha, kukamiliaka kwa kazi yake iliyomleta duniani ambayo ilikuwa ni ukombozi. Kumweka huru kila mtu ili asipotee, bali awe na uzima wa milele. Kwa maelezo mengine tuseme kuwa, Msalaba wa Yesu, ulibadirisha Historia ya Ulimwengu wote na kuweka utamaduni mpya.
Msamaha wa dhambi ulitolewa; kupitia mauti ya msalaba wa Yesu, msamaha wa dunia ulitangazwa. Kupitia kifo cha msalaba, toba kwa ulimwengu ilipatikana. Kifo cha msalabani, kinatupa maji ya uzima, kinatupa pumziko la kweli, kina tuhesabia haki. Wakati wayahudi walidhani wanakomesha, kumbe agano la Mungu linatimia kwa ulimwengu, kuwa Mtu hatafika mbinguni ila kwa njia ya Yesu Kristo. Kupitia kifo cha Yesu, mlango wa kuiendea mbingu ilifunguliwa wazi kwa wote wampokeao na makao yao yakaanza kuandaliwa tangu hapo. Hata leo, ukiokoka, makao yako yanaanza kuandaliwa leo.

MAOMBICIMG7615.JPG
Ndugu yangu, natumai umesoma ujumbe huu, leo Roho wa Mungu amenituma kwako, nikuueleze habari hii ya Msalaba, sijui umeteseka kwa kiwango gani katika hali hiyo uliyonayo, wala sijui hamu yako ya kumtumikia Mungu inalinganaje, wala sifahamu umesongwa kwa kiwango gani, pengine umefikia hatua ya kukata tamaa, huoni msaada utatoka wapi, lakini ujumbe huu umefika kwako muda huu; upo msaada usioisha,upo uweza usioshindwa, ipo nguvu isiyoteteleka, nayo ni nguvu ya Msalaba wa Yesu Kristo, aliye chukua laana na uovu wetu ili tupate kuwa huru. Aliyechukua dhambi zetu, aliyebeba magonjwa yetu, huzuni zetu na kila adha; unapo pata habari hizi, nakusihi sana usikubali kuendelea kukaa katika vifungo hivyo, toka gerezani, Mungu amekukumbuka, amekuona,usifanye moyo wako kuwa mgumu, jiachilie kwake uwe huru, kwa Jina la Yesu Kristo. Pokea kwa kadri ya uhitaji wako, unayetaka mwenza, unayetaka mtoto, unayetaka kuinuliwa katika masomo, usiye na kazi, unayeteswa na madeni, kila kona unavutwa shati, kwa Jina la Yesu, unayeonewa kazini kwako, umeshushwa cheo, umeonewa vya kutosha, kwa Jina la Yesu, pokea uweza mpya na nguvu mpya. Uwe huru sasa, ufurahi tena, ububujike amani tele moyoni, kwa Jina la Yesu Kristo.

Kama unahitaji kuokoka, au ungependa kupata ushauri wowote maombezi au kutoa ushuhuda, wasiliana na
                       272350_106794086085746_2849313_o.jpg                                                                                                                             Sospeter.JPG
Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.
Kwa Mobile +255(0)7 (57/84) 464 141/ 12 909 021.
Tunakushauri, utembelee kanisa la kiroho lililo jirani yako, kwaajili ya mafundisho zaidi na Ushirika. (Kumbukumbu la Torati 28:6).

Oval:  
YESU NI
BWANA