Shemu ya Tano
Jambo la Tano
Uamuzi wa kuoa au kuolewa, unaweza ukabadilisha
utumishi wako na wito wako kabisa
Uamuzi wa kuoa au kuolewa, unaweza ukabadilisha
utumishi wako na wito wako kabisa
Ngoja nikutolee mfano wa kibiblia.
Unamkumbuka mtu mmoja aliyeitwa Samson, alimwoa dada mmoja aliyeitwa
Delila, utumishi wake ulinyongewa huko kwenye maisha yao ya ndoa. Ukisoma kile
kitabu cha Waamuzi.16:21 kinasema hivi, “Wafilisti wakamkamata wakamng’oa
macho, wakateremka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba naye
alikuwa akisaga ngano katika gereza”.
Unajua huyu alikuwa ni mtumishi wa Mungu
mzuri kabisa. Lakini hakujua ya kwamba yule mwanamke aliyempenda na akamwoa
aishi naye alikuwa ni ‘ajenti’. Hakujua ya kuwa yule dada alikuwa ni
‘ajenti’ wa adui. Yule dada alikuwa ni ‘ajenti’; kabisa akambembeleza mume wake
amweleze siri ya nguvu zake, lakini Samsoni mwenyewe alikuwa anaficha kusema
siri ya nguvu zake iko wapi. Lakini yule dada alikuwa na ujuzi wa kubembeleza.
Akambembeleza yule baba kiasi ambacho akashindwa kuficha siri yake, na
akaisema.
Unajua inapofika kwenye masuala ya ndoa
inatakiwa muweze kusaidiana, mtu asitumie udhaifu wako kukuangusha, mtu
asitumie udhaifu wako kukuzamisha, mtu asitumie makosa yako kukupeleka
jehanamu, inatakiwa ukimpata mwenzako ukiwa na udhaifu akusaidie, ukiwa kwenye
dhambi akuombee utoke, unaelekea jehanamu akusaidie kwenda mbinguni, ndivyo
inavyotakiwa iwe kwenye ndoa.
Lakini ninakuambia ukimpata mtu, na wewe una
maisha yanayoelekea jehanamu, anakuambia nenda salama, hii ni hatari.
Yule dada alikuwa anamfuatilia Samsoni kumnyang’anya kitu kilichokuwa ndani
yake cha utumishi alichokuwa amepewa na Mungu, na Samsoni hakujua. Alipofika
mahali pa kuisema siri yake alifikiri mke wake ni mwenzake ambaye anaweza
akampa siri yake vizuri bila shida.
Ndio maana kwenye ndoa ambazo watu
hawaaminiani vizuri, siri zao hawaambiani. Na ikishafika kwenye ndoa, mnasiri
mlizozifichana iko shida, maana yake kuna eneo ambalo usingetaka liingiliwe,
unafunga na ufunguo, kasha unatembea na ufunguo mfukoni. Ni eneo umeficha,
kwenye ndoa mnatakiwa mfahamiane kila siku, na udhaifu wako, na shida ilioko,
na matatizo yaliyoko, kila kitu kiwepo peupe, ili mwenzako atafute namna ya kukusaidia.
Samsoni aliona kitu cha tofauti, lakini
alikuwa mke wake, maadui wakaja wakamshika, mke wake anatazama na kushangilia.
Badala ya Samsoni kumtumikia Mungu, akaenda akawa anasaga ngano gerezani.
Biblia inasema wakamtoboa macho. Kwa jinsi ya rohoni ningekuambia,
wanaondoa macho yako ya rohoni, maono ya Kimungu yanapotea, mtazamo wa Kimungu
unapotea, mipango ya Kimungu inapotea.
Ndio maana unakuta mtu ameolewa ameokoka, au ameoa huku ameokoka,
akifika ndani ya ndoa maono ya Kimungu yanapotea, na utumishi wake
unazama. Anabaki kusema ‘Bwana asifiwe’, kama bado anaweza akaendelea
kusema ‘Bwana asifiwe’, lakini ndani ya moyo amenyonywa kiroho na hakuna kitu.
Sasa labda na ninyi ni mashahidi, wewe angalia vijana ambao wameoa
na kuolewa, angalia kama bado wanao moto ule ule wa utumishi, ambao walikuwa
nao kabla hawajaingia kwenye ndoa. Wengine wanabaki kumsingizia Mungu ya
kuwa, ameesbadilishia huduma, wakati sio Mungu, kumbe ni mume wake
amembadilishia huduma, au ni mke wake tu amembadilishia huduma! Maana
hakuhesabu gharama ya ndoa kwenye wito wake.
Kwa mfano; Mke wako anakutaka nyumbani, huduma inakutaka
kila siku uwepo barabarani, usije ukafikiri ni kitu kirahisi hicho. Utafika
mahali lazima uamue, unataka kumpendezesha mke wako au unataka kumpendezesha
Mungu.Haya si mambo ambayo ni rahisi kuyaweka vizuri na kuyaanisha bila msaada
wa Mungu. Na kama alikuwa anajua anaolewa wapi, kusumbuliwa suala la kusafiri
kwako kwenye huduma lisingekuwepo, angekua anakutia moyo na kukuombea, na
kukusindikiza siku nyingine. Lakini inapofika anaanza kupata shida, maana yake
kuoana kwenu kuna kasoro mahali, na kumekuwa mzigo.
No comments:
Post a Comment